SHUGHULI ZA UWEKEZAJI WILAYA YA MBULU
Maeneo ya uwekezaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeainisha aina na maeneo ya uwekezaji kuwa ni Uzalishaji na usindikaji wa matunda, Uzalishaji na usindikaji wa mazao ya viungo, Uzalishaji wa mpira, Utalii, Hoteli na Uvuvi.
1. Uwekezaji katika kilimo
Kilimo cha mazao ya chakula na biashara ni fursa zinazopatikana Wilaya ya Mbulu, Wilaya ya Mbulu ni maaarufu kwa ulimaji wa :
Shamba lina ukubwa wa Hekta 3,036.36 na limepimwa, eneo la ardhi lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji ni Hekta 892.1 na utaratibu wa uwekezaji utakaotumika ni ubia au Kuuza.
Viungo vinavyostawi katika Wilaya ya Mbulu ni Iliki, Mdalasini, Karafuu, Pilipili manga na Kakao. Uzalishaji na uuzaji wa viungo ni wa chini ingawa kuna maeneo mazuri ya uzalishaji. Kuna ukuaji mkubwa wa mahitaji ya mazao ya viungo duniani ikiwa uzalishaji utakuwa na ubora hasa kilimo kisichotumia mbolea za viwandani. Soko la nje ni kama Afrika ya kati, Asia, Ulaya, Afrika na Amerika. Soko la ndani linajumuisha Zanzibar na Tanzania Bara.
Eneo lililotengwa ni Kihuhwi shamba la Bwembwera lenye ukubwa wa hekta 2,300. Uzalishaji wa mpira kibiashara bado haujaendelezwa hapa Tanzania kiujumla, Uzalishaji wa Mpira katika Tarafa ya Bwembwera ni mkubwa na kama utaendelezwa bidhaa nyingi zinazotokana na mpira zitazalishwa.
2. Uwekezaji katika sekta ya Viwanda
Kupitia makongamano ya Uwekezaji ambapo fursa za uwekezaji zilitangazwa na Wawekezaji walionesha nia ya kuwekeza katika Halmashauri, hadi sasa hatua zilizofanyika ni kuenga eneo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha kusindika mhogo kwa mwekezaji Community Money Transfer Limited (CMTL). Mwekezaji anaendelea kufuatilia upatikanaji wa fedha (Capital) kutoka UN na kufanya utafiti juu ya takwimu za uzalishaji wa machungwa ambapo Sampuli za machungwa zimechukuliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini ubora wake ambapo imeonekana kuwa machungwa ya Mbulu yanafaa, aidha mazungumzo juu ya uwekezaji huo yanaendelea kufanyika baina ya MUVI kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na mwekezaji (Teampro - Muungano wa Makampuni ya Uholanzi).
3. Utalii wa Ikolojia na wa Kiutamaduni
Yapo maeneo kadhaa ambayo ni vivutio vya aina hii ya Utalii. Maeneo hayo ni pamoja na hifadhi ya asili ya Amani ambapo wanapatikana viumbe adimu ulimwenguni, vivutio vingine ni ufugaji wa vipepeo eneo la Amani, Maporomoko ya maji ya Mto Zigi, Ua la St Paulia, Mlima wa Mlinga, kanisa la kwanza la Angalican katika Tanzania- Utalii unajumuisha maeneo mazuri ya fukwe yaliyopo katika kata ya Kigombe. Uwekezaji katika sekta hii ni muhimu ili kukuza sekta ya utalii. Hii inajumuisha ujenzi wa hoteli za kitalii na ufugaji wa vipepeo.
4. Uwekezaji katika sekta ya uvuvi
Katika Wilaya ya Mbulu shughuli za uvuvi zinafanyika katika bahari ya Hindi eneo la Kigombe. Uzalishaji wa samaki katika eneo hili ni mkubwa na unahitaji kuendelezwa. Uvuvi katika Wilaya ya Mbulu unahusisha uvunaji wa samaki katika mabwawa, hivi sasa yapo mabwawa 84 yanayotumika kati ya mabwawa 128 yaliyopo. Hata hivyo ufugaji unaofanyika katika mabwawa kwa sasa ni kwa ajili ya matumizi ya chakula kwa mfugaji husika (Domestic use). Endapo mabwawa haya yataendelezwa uzalishaji wa samaki utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Vichocheo katika uwekezaji huu ni kuwepo kwa miundombinu ya barabara (Barabara ya Tanga- Kigombe- Pangani), aina za samaki zilizopo na bwawa jipya la Misozwe ambayo yana nafasi kubwa ya uendelezaji.
5. Uwekezaji katika Sekta ya Huduma
Wilaya inayo maeneo ya yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa huduma za jamii ikiwemo Viwanja kwa ajili ya Ujenzi wa Shule za Sekondari na chuo kikuu. Eneo lipo lenye ukubwa wa Ha 5.3 na limefanyiwa upimaji wa awali (Dermacation) na katika shamba la chartur lipo eneo la ujenzi wa chuo kikuu. Eneo lenye ukubwa wa Ha. 2 limefanyiwa upimaji wa awali (Dermacation) lipo katika Kata ya Kwemkabala na Ha. 1.5 lipo katika Kata ya Magila, Kijiji cha Mkwakwa Mafleta.
6. Eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya
Eneo lenye ukubwa wa Ha. 1 lipo katika Kata ya Kilulu na limefanyiwa upimaji wa awali (Dermacation).
Maeneo kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba za makazi (Housing Estate) yapo mawili; eneo la Chartul lenye ukubwa wa Ha 1.7 limeshapimwa na upimaji wa awali (Dermacation) umefanyika, na Ha 1.4 zimetengwa katika eneo la Kwemkabala
Kusoma zaidi Makala ya Maeneo ya Uwekezaji wilayani Mbulu
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.