Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu limepitisha na kupongeza rasimu ya mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika kikao chake cha kawaida ikiwa 41,462,135,600 imependekezwa, baada ya kujadili kwa kina vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Chama Tawala pamoja na miongozo ya Serikali. Kupitishwa kwa rasimu hiyo kunalenga kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuchochea maendeleo endelevu ndani ya Halmashauri ya Wilaya.
Rasimu ya mpango na bajeti hiyo imezingatia maeneo muhimu ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya na maji, ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara, pamoja na kuimarisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi.
Aidha, mpango huo umejikita katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati itakayoongeza fursa za ajira, kukuza kipato cha wananchi na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Yeconia Deless amewapongeza madiwani kwa ushiriki wao katika majadiliano na kusisitiza umuhimu wa usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa miradi itakayotekelezwa chini ya bajeti hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Juma Kilimba ameahidi kuwa menejimenti itazingatia matumizi bora ya rasilimali, uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa mpango na bajeti, huku akisisitiza kuwa maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Baraza yatazingatiwa kikamilifu pia halmashauri itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wote kwa usawa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.