• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Mahafali ya Kidato cha 4 Shule ya Sekondari Philip Marmo Yafana, Huku Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A.Kuuli Akiahidi Kuzitatua Kero Mbalimbali za Shule Hiyo Tarehe 15.10.2021

Kurushwa hewani: October 16th, 2021


Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akizungumza Katika Mahafali Hayo.

Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akiingia Shule ya Sekondari Philip Marmo Akipokelewa na Wenyeji Wake Mkuu wa Shule Bw. Edmund E. Obed na Afisa Mtendaji wa Kata ya Endamilay (wa kike kushoto) Bi. Natalia Julius.

Wanafunzi wa Kidato cha 4 Wakiingia kwa Muziki Maalumu Eneo la Sherehe Katika Mahafali Hayo Shule ya Sekondari Philip Marmo.


Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akisoma Vitu Mbalimbali Katika Mahafali Hayo.

Wanafunzi wa Kidato cha 4 Katika Mahafali Hayo.Wananchi Wakiwa Katika Mahafali Hayo.

Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikagua Kikosi cha Skauti cha Shule Hiyo.

Bw. Mussa Mpinga Mzee Aliyewawakilisha Wazazi kwa Upande wa Wanaume Kuzungumza Neno la Heri kwa Niaba Katika Mahafari Hayo.

Bi. Pepetua Philipo Aliyewawakilisha Wazazi kwa Upande wa Wanawake Kuzungumza Neno la Heri kwa Niaba Katika Mahafari Hayo.

Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Ukakamavu wa Skauti katika Kusimamisha Pikipiki Kutokutembea.




Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kucheza Muziki wa Miondoko ya Kizazi Kipya.


Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kitaaluma Namana ya Kutambua Chakula Kama Kina Protini Kwa Kutumia Vifaa Maalumu Vya Somo la Kemia Wako Vizuri kwa Kweli na Hii ni Pongezi Kubwa Sana kwa Waalimu. 

Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kucheza Muziki wa Mirindimo ya Kitamaduni Zaidi.


Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Skauti wa Mbele ni Kiongozi Wao Foibe D. Joseph.


Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Zawadi ya Tsh. 120,000/= kwa Wanafunzi Hao Walionyesha Michezo Mbalimbali.

Wanafunzi Wakibeba Keki .

Wanafunzi Wakikabidhi Keki kwa Mkuu wa Shule Bw. Edmund E. Obed


Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Alivishwa Vazi la Heshima la Kimila na Fimbo ya Kimila ya Kiiraq.

Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Cheti cha Pongezi kwa  Mkuu wa Shule ya Philip Marmo Bw. Edmund E. Obed.



Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Cheti cha Pongezi kwa  Mwalimu wa Michezo Bi. Doroth Baraka wa  Philip Marmo.


Wanafunzi Wakikabidhiwa Vyeti.




Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Katika Picha ya Pamoja Waalimu na Wanafunzi.


Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akiondoka Baada ya Kuisha Mahafali Hayo.




~~~~~~~~~~~        HABARI KAMILI       ~~~~~~~~~~~





Haya yamejiri jana katika mahafali yaliyofana kwelikweli kwa kuambatana na maonyesho mbalimbali ya vichekesho na kuelimisha umma kama vile igizo lililo elimisha wazazi kutoendelea kushikilia mila na desturi potofu za kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo na kuacha masomo, pia ukeketaji ambao humuathili mwanamke katika uzazi namna ya kujifungua kwa kupata maumivu makali na kutokwa na damu nyingi na hata kupelekea kifo.


Onyesho la kitaaluma lililowahusisha wanafunzi 5 ambao waliandaa jaribio la namna ya kutambua kama chakula husika kina protini jambo ambalo lilithibitika baada ya mchanganyiko wa kemikali kadhaa na chakula husika kuonyesha rangi ya bluu iliyokolea.  Huu ni uwezo tosha kwa wanafunzi hawa kuwa wataalamu wa kuchambua vyakula mbalimbali vinavyotumika na binadamu ili kujua kama vina madhala au la!


Maonyesho ya ukakamavu ya kikosi cha skauti yaliyofundisha kwamba kila jambo likifanyiwa kazi vya kutosha kwa kujituma basi linawezekana kufanikiwa, imefahamika wazi kwamba vipaji vya watoto kutoka kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Sekondari ya Philip Marmo ni vya kiwango cha juu kabisa.

Shule ya Sekondari Phili Marmo iko kata ya Endamilay na ilikuwa na wanafunzi 82 kutokana na sababu mbalimbali imepelekea hadi sasa kuwa na wanafunzi 75 ambao ndiyo watakaofanya mtihani wao wa kitaifa wa kidato cha 4 katikati ya mwezi Novemba 2021.


Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar A.Kuuli amesifu vipaji mbalimbali walivyonavyo wanafunzi hawa na kutamka viendelezwe, hakuishia hapo tu aliwatunuku kiasi cha Tsh. 120,000/= kwa wanafunzi 12 wa uimbaji. Lakini amewashukuru waalimu wote walioshiriki katika uleaji wa vipaji hivi kwani ni hazina kubwa kwao na jamii kwa ujumla. Kwa sasa uwekezaji katika michezo, burudani na sanaa za maonyesho ni sehemu tosha ya kujipatia kipato cha juu kama ilivyo kwa watu mbalimbali waliofanikiwa kupitia kada hizi hivyo wasikate tamaa.


Mgeni rasmi huyo aliendelea kusisitiza kwamba "ni lazima wanafunzi kuwa na tabia njema ndiyo mwanzo mzuri wa mafanikio yoyote, hivyo muepuke kuwa wezi, wabakaji, tabia mbaya  na kuwasaidia wazazi katika kazi mbalimbali pale inapofaa kufanya hivyo, lakini pia mshikeni sana MUNGU kwani yeye ndiyo kila kitu" alisisitiza.


Kuhusiana na changamoto za maabara, bweni na bwalo Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar A.Kuuli amesema atamtuma Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Mbulu kuja kufanya tathmini ya kiasi gani kinahitajika katika kila mradi na litaandikwa andiko kwenda kwa wadau mbalimbali kama vile (TEA) wanaotusaidia katika fedha mbalimbali za Elimu, pia kwa ujio wa Mhandisi atasaidia kazi zilizokuwa zimesimama kwa muda mrefu ziweze kuendelea, kwani fedha zipo. Mhandisi atakuja wiki ijayo kuanzia tarehe 18.10.2021 lakini kuhusu maji atawasiliana na Meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini (RUWASA) ili nao wafike wafanye tathmini kisha tutajua tutakabiliana vipi na hiyo gharama itakayoletwa ili maji yafike hapa Shuleni Philip Marmo sekondari.


Hata hivyo ukosefu wa vifaa TEHAMA kama vile kompyuta (Tarakilishi)  na printa (kinakilishi) kwa ajili ya kufanyia kazi mbalimbali za kimfumo kuanzia FFARS mfumo wa malipo, PREM usajili wa wanafunzi na SELFOM mfumo wa uhakiki wanafunzi hususani katika ngazi ya kufanyia mitihani. Katika kujibu hili hapa Mgeni rasmi alitamka kwamba fedha elimu bure zinazoingia kila mwezi basi waangalie namna ya kutumia fedha zile katika ununuzi wa Vitanda na vifaa tehama hivi lakini na yeye atasaidia ununuzi wa PRINTA.  


Mgeni rasmi huyo alitamka kwamba "mtoto yeyote wa kike ambaye atashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa fedha za kuendelea na elimu yake basi afike kwa Mkuu wa shule hii kisha mimi Mkurugenzi mwenyewe nitaangalia namna ya kumsomesha mwanafunzi huyo". 

Mgeni rasmi amewashukuru wanafunzi, wazazi, viongozi wa dini, chama, waalimu na wanafunzi kwa ujumla wao kwa ushiriki wao katika mahafali haya.














Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.