• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

MIRADI YA BILIONI 1.8/- YAPITIWA NA MWENGE WA UHURU MBULU DC .

Kurushwa hewani: October 12th, 2023

Na Ruth Kyelula, Mbulu DC.

   

Miradi saba yenye thamani ya Bilioni 1,878,743,413 imefikiwa na mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.

Hayo yalibainishwa mnamo tarehe October, 11, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara Kheri James, mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim.


Komred Kheri alisema Mwenge ulipokuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu umekimbizwa katika miradi saba yenye thamani ya Bilioni 1.8 na kukimbizwa katika umbali wa kilometa 100.3.

Aidha, alisema kati ya miradi 7, miradi mitatu imezinduliwa ambayo ni pamoja na mradi wa Maji Labay ambao umegharimu kiasi cha sh.1,069,270,393, ujenzi wa daraja la Barazani ambao umegharimu 249,980,000, na mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Msingi Flatei Massay iliyopo Haydom ambao gharama zake za ujenzi ni sh.348,500,000 kutoka serikali Kuu na nguvu ya wananchi ni milioni 17,500,000 ambapo inafanya jumlya yake kuwa Milioni 366,000,000.


“Pia Mwenge wetu wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu utafanya kazi ya kuona miradi miwili ambayo ni Uhifadhi wa chanzo cha maji Maghang, pamoja na kuona mradi wa karakana ya vijana ya kuchomelea vyuma,”Alisema Komred Kheri James.

Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Wilaya hiyo, umefanya kazi ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa wa Ujenzi wa Zahanati  katika kijiji cha Harsha pamoja na mradi wa Soko la mboga mboga uliopo katika kata ya Dongobesh.

Mkuu wa Wilaya alifafanua kuwa katika Utekelezaji wa miradi hiyo Serikali Kuu ilichangia jumla y ash. Bilioni 1,717,750,393, ambapo Halmashauri ya Wilaya hiyo imechangia miradi mitatu, Ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Harsha kwa kuchangia sh.Milioni 24.2, mradi wa karakana ya vijana ya kuchomelea vyuma kwa kuchangia sh.Milioni 5,554,445. Aidha alisema pia Halmashauri ya Wilaya imechangia katika ujenzi wa Soko la Mboga mboga kwa kuchangia sh. Milioni 93,948,375 na kupelekea jumla ya sh. Milioni 123,702,820.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa Komred Kawaida alisema kuwa yapo mambo mengi ya msingi na muhimu ambayo Mheshimiwa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hasan anafanya kwa vijana wa kitanzania,ikiwemo mikopo ya asilimia 10, 4% kwa vijana, 4% kwa kinamama na 2% kwa watu wenye mahitaji maalumu lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi.

 

“Niwaambieni tunatambua mtihani tulionao sasa kwamba mikopo hii imesitishwa, niwatoeni hofu kuwa serikali inayo nia njema ya kuhakikisha mikopo hii inawafikia moja kwa moja walengwa ikiwa na maana kina mama, Vijana na Watu wenye mahitaji maalumu.”Alisema Kawaida.

Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa mbio za Mwenge za mwaka 2023 zimefika katika mradi  wetu wa kikundi cha Vijana, kwanza kabisa Mwenge wa Uhuru kama ilivyokawaida tumepokea taarifa inayohusiana na mradi, tumefanya ukaguzi wa nyaraka, tumetembelea, tumekagua na kujionea shughuli ambazo kimsingi zinafanywa na vijana wetu.


"Ndugu zangu wapendwa  niwaambie kwa dhati kabisa baada ya ukaguzi wa kina ambao tumefanya kwa upande wa nyaraka tumejiridhisha tumeona shughuli ambazo kimsingi vijana wetu wanafanya, tumeridhia shughuli wanazozifanya vijana wetu, nichukue fursa hii Mheshiwa Mkuu wa Wilaya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa namna ya pekee mnavyoendelea kutoa mikopo hii  kama programu ya kufuata na kutekeleza  maagizo ya Serikali kwa lengo la kuwezesha wananchi kupitia programu ya 442, asilimia 4 Vijana, 4% Wanawake na 2%  kwa watu wenye mahitaji maalumu. Hongereni sana kwa kazi mliyoifanya." Alisema Kaim.

Aidha Kaim alisema kuwa  vijana wajitahidi kutumia fedha hizo kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama sehemu ya kujiajiri na kukuza kipato chao, pia amewashukuru vijana hao kwa kuwa wazalendo kwa kukamilisha marejesho ya mikopo yao . Amemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia vijana hao kupata mafunzo Ili bidhaa wanazotengeneza ziwe na ubora na viwango zaidi. Lakini pia muwasaidie katika upatikanaji wa tenda pamoja na mambo mengine.

#KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.