• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

MWEKEZAJI MBULU APEWA EKARI 988.

Kurushwa hewani: March 11th, 2018

Halmashauri ya Kijiji cha Eshkesh kilichopo katika kata ya Eshkesh  Wilayani Mbulu Mkoani Manyara ilipokea ombi la Ardhi yenye  ukubwa wa ekari 7000 kutoka kwa kampuni ya Bargweka Farm Ltd.mnamo tarehe 08/04/2010 kwa ajili ya ufugaji ng’ombe wa kisasa aina ya“Boran”

Baada ya ombi hilo kuwasilishwa, halmshauri ya kijiji na mkutano Mkuu wa kijiji cha Eshkesh viliridhia kampuni ya Baragweka ipewe ekari 3903 badala ya ekari  7000 ambazo mwombaji alikubaliana na kijiji atatoa huduma za jamii kama vile maji,mojosho,mashine za kusaga nafaka, zahanati na shule.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya vijiji Na.5 ya mwaka 1999  ombi hilo liliwasilishwa kwa Halmashauri ya Wilaya na hatimaye kwa kamishina wa Ardhi Msaidizi kanda ya kaskazini kwa hatua zaidi za kwa Mhe. Waziri wa Ardhi,Nyumba naMaendeleo ya  Makazi. Wakati Waziri akiwa kwenye mchakato mzima wa uhawilishaji alipokea malalamiko kuhusu mchakato mzima wa uhawilishaji wa eneo hili na alisitisha uhawilishaji mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Baragweka Farm Ltd. Alipeleka malalamiko kuhusiana na kusitishwa kwa mchakato wa uhawilishaji wa eneo hilo kwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhauri wa Muungano wa Tanzania, ambapo Waziri Mkuu aliunda timu ya wataalam kufuatilia malalamiko hayo mnamo mwezi Mei,2017.

Baada ya timu kupitia malalamiko hayo waliweza kubaini kuwepo kwa mapungufu mengi  na Mhe. Waziri Mkuu alitoa maagizo kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara,Kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa Wilayani Mbulu mwezi februari 2018 . Timu ya Wataalam wa ardhi kutoka ofisini kwake wakishirikiana na wataalam wilayani hapo waliombwa kupitia mchakato huo upya kama iliyoagizwa na Waziri Mkuu. Mchakato uliopitiwa na timu hiyo   ulizingatia mapitio ya Mpango wa matumizi bora ya ardhi na kujadili maombi ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa shamba la mifugo katika kijiji cha eshkesh.

Kufuatia kikao cha Baraza maalum la Madiwani lililokaa mnamo tarehe 09/03/2018, baada ya kukaa na kujadili kwa zaidi ya masaa matatu kuhusiana na mchakato uliopitiwa,Madiwani waliohudhuria kwenye kikao hicho maalumu walikuwa madiwani wapatao 23 ambapo waliweza kuhitimisha kwa kuzingatia muongozo na kuhamua kupiga kura, ambapo Madiwani 14 walisema mwekezaji wa kampuni ya Bagweka Farm Limited apewe ekari 988 badala ya ekari 3,903 zilizoombwa.

Aidha Madiwani 6 walisema mwekezaji wa kampuni ya Bagweka Farm Limited apewe ekari 3,903, badala ya ekari 988.

Kikao hicho maalumu cha madiwani kimefanyika kwa agizo la mkuu wa mkoa wa manyara bwana Alexanda Mnyeti ya kutaka kujadali namna ambavyo mwekezaji aliwasilisha malalamiko yake katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.