• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

WALIOFARIKI KATESH WAFIKIA 63, MAJERUHI 116

Kurushwa hewani: December 5th, 2023

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo wilayani Hanang, mkoani Manyara imefikia 63 na majeruhi 116.

“Kati ya waliofariki wanaume ni 23 na wanawake ni 40. Miongoni mwao, watu wazima ni 40 na watoto ni 23. Kwa watu wazima, wanaume ni 14 na wanawake ni 26; kwa watoto, wa kiume ni tisa na wa kike ni 14,” amesema.

  “Majeruhi ni 116 ambapo wanaume ni 56 na wanawake ni 60; miongoni mwao watu wazima ni 60 na watoto ni 56. Kati ya watu wazima 60, wanaume ni 29 na wanawake ni 31 wakati watoto waliojeruhiwa, wa kiume ni 27 na wa kike ni 29,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo kwa Taifa leo (Jumatatu, Desemba 4, 2023) kabla ya kuongoza mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho kwenye ibada ya kuwaaga marehemu hao katika uwanja wa shule ya msingi Katesh ‘A’ wilayani humo.

 

Ibada ya kuwaaga marehemu iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Manyara, Sheikh Mohammed Kadidi pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Baba Askofu Anthony Gaspar Lagwen ambaye alisema Kanisa hilo litachangia sh. milioni tano kwenye mfuko wa maafa.

  

Akizungumza na waombolezaji hao, Waziri Mkuu aliwafikishia salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwajulisha kuwa ametoa maelekezo kwamba Serikali isimamie kwa namna yoyote ile masuala ya wafiwa na majeruhi na kuhakikisha kuwa wote walionusurika wanahudumiwa.

“Mheshimiwa Rais ameelekeza kwamba huduma za miili itafanywa na Serikali kwa kutoa majeneza na usafiri hadi makwao ili kila mmoja akazikwe kwa taratibu za kimila na kifamilia. Kwa majeruhi wote, matibabu yatolewe bure hadi wapone na kurejea kwenye hali zao,” amesema.“Mbali na majeruhi, kuna watu nyumba zao zimesombwa; hawa ameelekeza wawekwe kwenye kambi maalum, ambazo nimeambiwa ni shule tatu na wapewe chakula, maji na huduma za matibabu endapo italazimu.”

 

 Waziri Mkuu amesema leo imeagwa miili ya watu 52 ambayo tayari ilikuwa imeshaandaliwa na kesho asubuhi (Desemba 5, 2023) litafanyika zoezi la kuaga miili iliyobakia. Alisema ili kuwe na uratibu mzuri, taarifa za kila siku kuhusu tukio hilo, zitatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bi. Queen Sendiga na kwamba rambirambi zote zielekezwe kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

 

 

Kabla ya kushiriki kuaga marehemu hao, Waziri Mkuu alikwenda kukagua sehemu ambayo imeathirika zaidi ambako nyumba zote za kijiji cha Gendabi zilisombwa na maji na kubakizwa Kanisa tu. Pia alikagua kwa helikopta na kujionea athari za mafuriko hayo kwenye mji mdogo wa Katesh. Maeneo mengine yaliyoathirika ni Jorodon na Ganana.

 

 Amezishukuru Kamati za Maafa za Wilaya na Mkoa ambazo zilianza kuchukua hatua za uokoaji tangu jana, lakini pia mawaziri na watendaji wao ambao walikuja kutoa msaada kwa kuungana na viongozi wa mkoa wa Manyara.

 

Mapema, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Annamringi Macha aliwasilisha salamu za pole na kusema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa maafa hayo.

 Alisema wamekabidhi mchele (magunia manne) maharage (magunia 9), unga wa sembe (viroba 100 vya kg.25), katoni za maji 150 na sabuni ambavyo vyote alisema vina thamani ya sh. milioni 10.

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.