Kwa: WAZABUNI
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inapenda kualika zabuni kutoka kwa watu Binafsi, Makampuni, Ushirika, Taasisi au Vikundi vya watu vilivyosajiliwa kisheria wenye nia, uwezo na uzoefu wa Ukusanyaji wa Ushuru wa Mazao ya Kilimo kutuma maombi yao kwa Zabuni hii.
1.Unaalikwa kuwasilisha Zabuni yako kwa ajili ya kukusanya Mapato ya Ushuru wa mzazao ya KIlimo kama ilivyoainishwa kwenye Nyaraka za Zabuni.
2.Kotesheni inapatikana Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iliyopo Dongobesh, Barabara ya Dongobesh – Mbulu Mkabala na Njiapanda ya kwenda Haydom
3.Ada ya zabuni ni shilingi za kitanzania 200,000 (mia mbili elfu tu). Fedha hizi hazitarudishwa.
4.Zabuni zote zikiwa zimejazwa kikamilifu ziwasilishwe kwa MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU, S.L.P 74, DONGOBESH-MBULU kabla ya SAA 4:00 asubuhi tarehe 30 Mei 2022. Ufunguzi wa 5.Zabuni hizo utafanyika kupitia katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mara baada ya muda wa mwisho wa kuwasilishwa Zabuni.
6.Zabuni au sehemu za Zabuni ambazo zitawasilishwa kwa kuchelewa au zilizowasilishwa katika muundo usiokubalika hazitakubaliwa wala kuzingatiwa kwa ajili ya tathmini, bila kujali mazingira yoyote.
]IMETOLEWA NA
Abubakar A. Kuuli
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.