Seksheni hii inajumuisha na hospitali ya Wilaya, lengo la seksheni hii ni kusaidia au kuwezesha utoaji wa huduma bora za Afya za kinga, matibabu na maendeleo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii katika Wilaya.
Idara ndogo ndogo ndani ya Afya
Elimu ya Afya
Huduma za Tiba (Magonjwa ya ndani, Watoto, wajawazito, Upasuaji na Mifupa, Huduma za mionzi, Maabara na Mortuary)
Huduma za Kinga (Huduma za Afya ya mama na mtoto na Huduma za kuzuia magonjwa ya kuambukiza)
Utengemao (Rehabilitation)
Ustawi wa Jamii
Afya ya Mazingira
Majukumu ya Seksheni ya Afya na Ustawi wa Jamii
Majukumu ya Idara/Seksheni
Majukumu ya seksheni/sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii:
Kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa wa sera za Afya katika wilaya
Kuratibu masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii katika wilaya
Kusimamia utoaji sahihi wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali/vituo vya Umma na sekta binafsi katika wilaya
Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma za Afya
Kutoa ushauri wa kitaalamu katika uandaaji wa mipango ya upambanaji/uzuiaji wa tatizo la Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS)
kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na masuala ya Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS) katika wilaya
Kutoa huduma za Afya/msaada unaohitajika wakati wa milipuko ya magonjwa katika wilaya
Kutoa huduma za kliniki na matibabu kwa wagonjwa wa ndani na nje wanaoletwa kutoka vituo vya Afya/hospitali za mamlaka za serikali za mitaa
Kutoa huduma za kitaalamu (utaalamu wa kubobea) za matibabu
Kutoa/Kusaidia huduma za kitaalamu na msaada unaohitajika kwa vituo vya Afya na Hospitali za Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa milipuko ya magonjwa yakuambukiza
Kutoa huduma za rufaa za maabara na vipimo
Kuratibu upatikanaji wa madawa/vifaa tiba kwa ajili ya hospitali
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.