TAARIFA YA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU
UTANGULIZI
Idara ya maji inajukumu la kutekeleza shughuli mbalimbali za usambazaji wa maji safi na salama katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama ni asilimia 44.8%. Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya vituo vya kuchotea maji viapatavyo 371 kati ya hivyo vituo 259 vinafanya kazi kutoka katika vyanzo na miradi ya hapo chini;
S/N
|
Aina ya Vyanzo/miradi
|
Inayofanya kazi
|
Inayoendelea kujengwa
|
1
|
Malambo kwaajili ya mifugo
|
17
|
2
|
2
|
Visima virefu vyenye Pampu za mikono
|
88
|
|
3
|
Visima vifupi vyenye Pampu za mikono
|
27
|
|
4
|
Miradi ya maji ya mserereko
|
3
|
2
|
5
|
Miradi ya maji ya inayosukumwa kwa pampu/mashine /solar
|
7
|
1
|
6
|
Chemchemi zilizoboreshwa
|
9
|
|
7
|
Matenki ya uvunaji wa maji ya mvua
|
23
|
|
8
|
Mabwawa makubwa umwagiliaji
|
1 (mangisa)
|
1 (D’besh)
|
HALI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inatekeleza miradi tisa ( 8 ) kati ya miradi kumi na moja ( 10 ) ( ambapo katika vijiji viwili maji yalikosekana ) kwa mchanganuo wa hapo chini kama ifuatavyo;
MIRADI YA WSDP I INAYOTEKELEZWA NA WILAYA
|
IDADI YA VITUO VYA MAJI
|
IDADI YA WATU
|
|||||
IDADI
|
VIJIJI
|
ILIYOKAMILIKA
|
INAYO ENDELEA
|
HAIJA ANZA
|
VILIVYO JENGWA
|
VINAVYOFANYA KAZI
|
|
10
|
22
|
4
|
4
|
2
|
159
|
60
|
67,253
|
Thamani ya miradi ya vijiji kumi inayotekelezwa katika Wilaya yetu, fedha iliyolipwa kwa wakandarasi hadi sasa na fedha iliyobaki kukamilisha miradi inayoendelea kama ifuatavyo;
THAMANI YA MIRADI
|
FEDHA ILIYOLIPWA
|
FEDHA ILIYOBAKI
|
% YA FEDHA ZILIZOLIPWA
|
% ASILIMIA YA UTEKELEZAJI
|
6,531,999,594
|
3,622,052,238
|
2,909,947,356
|
55.5 |
78 |
WADAU MBALIMBALI WALIOSHORIKI ANA NA WILAYA YA MBULU KATIKA SEKTA YA MAJI
Katika ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya maji.
Washirika hao ni WaterAid Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Jimbo Katoliki la Mbulu (DMDD), TAG Jimbo la Mbulu, NCA kupitia 4CCP na KKKT Dayosisi ya Mbulu.
FEDHA ZILIZOTENGWA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Mwaka wa fedha 2015/16
|
Mwaka wa fedha 2016/17
|
||
BAJETI
|
ZILIZOTOLEWA
|
BAJETI
|
ZILIZOLETWA
|
1,007,159,860.00
|
684,297,957.00
|
2,452,035,000.00
|
196,113,732.00
|
USAJILI WA VYOMBO VYA WATUMIAJI MAJI ( COWSO )
Aidha katika kufanya miradi inakuwa endelevu idara ya maji inajukumu la kuunda na kusajili lakini kuhakikisha wanafanya kazi zao ipasavyo vyombo vya watumia maji (COWSOs)
Hadi kufikia March 2017, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeunda na kusajili kisheria vyombo vya watumiaji maji vipatavyo 16 ambapo vyombo huru 6 vimeundwa na vipo katika hatua ya kusajiliwa, mpango ni kuunda na kusajili Cowoso 60 hadi 2020/21.
Baada ya vyombo hivi kuundwa na kusajiliwa kisheria hukabidhiwa miradi ya maji katika maeneo yao ili kusimamia, kuendesha na kuendeleza miradi iliyopo kwa manufaa ya wananchi wote.
MPANGO WA MIAKA MITANO 2016/2017-2020/2021
Wilaya ya Mbulu imeadaa mpango wa maji na usafi wa mazingira wa miaka mitano kuanzia 2016/17 hadi 2020/21 na inategemea kutekelaza miradi mipya katika vijiji 40, miradi ya upanuzi katika vijiji 2 na kufanya ukarabati wa miundo mbinu ya maji katika vijiji 15 kupitia program ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya pili ( WSDP II ) kupitia mpango huu tunatarajia kuwa hali ya upatikanaji wa maji itaongezeka kutoka 44.8% ya sasa hadi 85% ifikapo juni 2021.
Objective
To provide backstopping expert services to LGAs in the development of Water sector
This Section performs the following activities:-
•Analyse, coordinate and advise on the implementation of Water Sector Policies in the Region;
•Build Capacity of LGAs in Water Sector;
•Liaise with the relevant authorities in the Central and Local Government on water sectors issues;•Develop and improve water and sanitation in the region;
•Facilitate, co-ordinate, monitor and regulate all private sectors that provide water services in the Region;
•Facilitate and coordinate Water and environment cleanness Team in the Region;
•Facilitate and advise LGAs to identify and establish of rural water bodies;
•Facilitate LGAs in preparation of guidelines for implementation and rehabilitation of water projects.
The Section is led by an Assistant Administrative Secretary.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.