Mbulu is a town in Tanzania and the capital of the Mbulu District. The town is inhabited by people that identify as Iraqw people. The Roman Catholic Diocese of Mbulu is also located in Mbulu.
Mbulu also (known as Imboru among the Iraqw speakers) is the town in Northern Tanzania. The town is the core of minority cushitic speakers (iraqw people) in Tanzania. The town was founded by Germans in 1907 when they colonizes former German East Africa (Tanganyika, Burundi and Rwanda). Mbulu climate favoured Germans, also the hospitality of the indigenous favoured them. Germans were less harsh to the Iraqw people than the rest Tanganyikans. Thus Iraqw were used by Germans on white collar jobs. Today most Afro-German with Tanzanian ancestry are Iraqw from Mbulu. The main economic activities in Mbulu are Agriculture and Trade. Mbulu area is one of the earliest Wheat growing Plantations. During the British regime, Mbulu peasants were able to form trade union, Particularly Mbulu Wheat Growers association (1923). Most Famous people born in Mbulu are:
RAMANI YA WILAYA YA MBULU KUOYESHA MIPAKA TUNAYOPAKANA NAYO.
CHIMBUKO LA WAIRAQ!
WAIRAQ au Wairaki ni kabila kubwa
linalozungumza lugha jamii ya Wakushi na
linalopatikana Mkoa wa Manyara wilaya za
Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha
katika wilaya ya Karatu.
Watu wa kabila hilo wanauhusiano wa asili na
makabila ya Gorowa, Burungi na Alawa ambao
wanaishi katika wilaya za Babati na Kondoa.
Historia kwa njia ya simulizi za makabila inasema
chimbuko la Wairaqw linatokana na kizazi cha
watu wa kale walivyokuwa wakiishi eneo la
Mesopotamia, Iraq.
Vita ya mara kwa mara ilisababisha watu hao
kuhama makazi yao ya asili katika karne ya nne
hadi ya sita baada ya kuzaliwa kwa Kristo.
Wairaqw walivuka bahari ya Sham kwa mashua
na kutua Ethiopia ambako waliishi kwa muda
kisha kuendelea kuhama kuelekea Kusini
Magharibi kupitia bonde la ufa kando ya Ziwa
Victoria na kuweka kambi eneo waliloona ni
salama.
Kwa kuwa ni watu wasiopenda vita waliendelea
kuhamahama wakikimbia vita vilivyoruka sehemu
mbalimbali walizojaribu kuweka kambi. Walipita
njia ya kati kupitia Iramba Mkoa wa Singida
Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa
ambapo walikutana na mapambano ya Wahehe,
Wangoni na Wazimba.
Hali hiyo iliwalazimu kubadilisha njia na kurejea
kuelekea Kaskazini hadi sehemu ya Kondoa
mahali panapoitwa Guser Tuwalay na kuishi eneo
hilo huku wakijishughulisha na ufugaji na kilimo
kidogo. Hata hivyo ilitokea kutokuelewana kati
yao na watu wa kabila la Wabarbaig jambo
lililosababisha vita.
Ingawa walikuwa waoga wa vita walikuwa na
silaha za kujihami dhidi ya vita. Walitumia mikuki
na mishale ya asili ilitengenezwa na miti
iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma
unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye
ncha kali na baadaye waligundua zana
zinazotengenezwa kwa kutumia udongo wa
mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali
kama tofali.
Hata hivyo Wairaq walishindwa vita na kukimbilia
karibu na mlima Hanang kisha wakagawanyika
wengine wakaelekea mlima Dabil hadi Guser na
Gangaru ambapo walifanya maskani. Wairaq
walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo,
ASILI YA JINA LA MBULU
Alfredo is with Philomena Buxay and 13 others.January 19
NINI ASILI YA JINA MBULU? IJUE HISTORIA YA JINA MBULU SASA!
Wakati Wairaqw wakiwa bado wanakaa ``Irqwar Da/aw`` yaani bado hata hawajaanza kuhamia maeneo ya Mbulu, kuna binti alikuwa anaitwa Imbori alipata mimba yaani Doroway.
Doroway ilikuwa inaleta unajisi ``meeta`` kwenye familia husika na katu binti hakuruhusiwa kuzaa nyumbani na hawezi kuolewa na Mwiraqw yeyote, hivyo ilibidi Imbori afukuzwe kwao salama yake ni aolewe na mtu wa kabila lingine yaani ``homo`` ambao mara nyingi ni wadatoga au wambugwe.
Lakini kulikuwa na taratibu za kufuata na ilikuwa hivyo pia kwa Imbori. Alipobainika anamimba, Imbori alinyolewa nywele na kupakwa majivu kichwani ikiwa ni utambulisho kuwa ana``doroway`` alipfungashiwa chakula ambacho mara nyingi huwa viazi au mahindi ya kuchoma (haya yalikwepo muda wote kutokana na hali ya hewa ya Irqwar Da/aw) na kuongozwa na kaka yake aliyekuwa anatembea mbele yake ili amkabidhi kwa ``homo`` yeyote atakayejitokeza kama anataka mke au chakula kikiisha afie hukohuko porini au aliwe na wanyama.
Wakafika sehemu inayoitwa Mantla ambapo ni njia panda moja inaelekea Murray na nyingine Kainam na kwa kuwa Nade Be/a ambaye ni mganga maarufu kutoka Manda do Bayo alikuwa anakaa Murray hawakuthubutu kupitia njia hiyo maarufu kama ``tlo/u /awaak`` ambayo pia ilikuwa njia ya wamasai waliokuwa tishio kwa wairaqw hivyo wakapita njia ya Kainam hadi Aya Ma/ami ambako alifanikiwa kumpata ``homo`` aliyemwoa akaondoka naye hadi Mbulu.
Alipokwisha kuolewa ile ``meeta`` ikaisha na ndipo ndugu zake (pengine hata yeye mwenyewe baadaye) kumfuatilia kwa njia aliyofuatana na huyo mume wake na kufanikiwa kumpata na hatimaye kumtembelea mara kwa mara.
Katika kumtembelea huko, walikuwa wakisema tunaenda kwa Imbori ``do imboru kawaan``na hatimaye pakawa maarufu kama kwa Imboru na hatimaye Imboru.
Wajerumani walipofika wakashindwa kutamka Imboru wakawa wanasema Mbulu na ndipo hatimaye jina Mbulu likawa ``official``
Ahsanteni!
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.