Na, Ruth Kyelula, Mbulu DC
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo, alisema kuwa lengo la kutembelea Kituo cha Afya Dongobesh ni kupeleka huduma kwa mama wajawazito na wale waliojifungua, ili kuhakikisha wanaona mkono wa Serikali, viongozi na watumishi wa Hamashauri.
Timu ya wataalamu, waheshimiwa Madiwani na Mbunge wa Mbulu vijijini watoa sadaka kwa wazazi wa Kituo cha Afya Dongobesh, Januari 30, 2025.
Hayo aliyasema Januari 30, 2025 wakati akikabidhi sadaka hizo kwa Kaimu Afisa muuguzi mfawidhi wa kituo cha Afya Dongobesh, Zenobi Lucas, na katika ziara hiyo aliambatana na waheshimiwa Madiwani, Mbunge, kaimu Mkurugenzi pamoja na wataalamu wa Halmashauri.
“Huu ni mchango ambao tumeuchangisha sisi wataalam,madiwani na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya kusaidia wakina mama waliojifungua katika kituo chetu cha Afya Dongobesh, tunajua wanamahitaji mengi kina mama na wanatoka katika maeneo mbalimbali na pia hawana uwezo wa kukidhi mahitaji yale ya msingi, kwa hiyo sisi tumeona ni vema tuwaletee haya mahitaji kwa ajili ya watoto wao lakini pia wamama wajawazito ambao wapo hapa”. Alisema Mwenyekiti wa Halmashauri Mandoo.
Mhe.Mandoo alisema vitu vilivyopelekwa ni pempasi za watoto pc 20, soksi za watoto pc 20, mafuta ya watoto pc 20, kofia za watoto pc 20, baby shoo pc 20, sabuni ya unga mifuko miwili, maternity pads dazani mbili, nguo za ndani pc 20 na sabuni ya mche box moja.
Naye Mbunge wa Mbulu vijijini, Flatei Massay, alisema kuwa kama Hamashauri wameona ni vema kuwapelekea vitu hivyo kama sadaka kwa jamii hitaji inayowazunguka.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi, Juma Kilimba, alisema kuwa ni kawaida na ni utaratibu wa Halmashauri kuwasaidia watoto,wakina mama na makundi mengine wanayohitaji msaada,kwa hiyo utaratibu huo utakuwa endelevu kwa makundi yote hitaji kwa Halmashauri yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.