MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA MBULU NA MAENEO MENGINE KUWA ANAPANGISHA VIWANJA VYA BIASHARA KATIKA MIJI YA HAYDOM (STENDI-7, SOKONI-46) NA DONGOBESH (STENDI YA ZAMANI-28, STENDI YA SASA-99 NA SOKONI-6) AMBAPO MWOMBAJI/MPANGAJI:-
ATATAKIWA KUNUNUA FOMU YA MAOMBI KWA KIASI CHA TSHS 10,000/=
ATAKAYEFANIKIWA KUPATA KIWANJA ATATAKIWA KULIPIA TSHS. 100,000/=KAMA GHARAMA ZA UPIMAJI
ATAKAYEFANIKIWA KUPATA KIWANJA ATATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA KIBANDA HICHO KUFIKIA 30/06/2019.
UJENZI WA KIBANDA UTAZINGATIA RAMANI NA MAELEKEZO YA HALMASHAURI
BAADA YA UJENZI KUKAMILIKA MWOMBAJI ATAINGIA MKATABA NA HALMASHAURI WA MATUMIZI NA USHURU WA KIBANDA HICHO.
MUDA WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU YA MAOMBI NI KUANZIA TAREHE 21/01/2019 HADI TAREHE 10/02/2019.
FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA OFISI YA KATA YA DONGOBESH/HAYDOM NA OFISI YA BIASHARA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA LEO TAREHE 21/01/2019 NA OFISI YA
MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA YA MBULU
MFANO WA FOMU YA MAOMBI NI KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.