Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu anapenda kuwatangazia wakazi wote wa Haydom kuwa kuanzia tarehe 18/11/2018 hakutoruhusiwa kufanya biashara eneo la stendi ya Haydom ila kwa masharti yafuatayo:
1. Bodaboda na Bajaji kubeba abiria/kupaki ndani ya stendi atatakiwa kulipia 300/= kwa siku.
2. Malori makubwa (semitraler) kuingia stendi kushusha na kupakia mzigo atalipa Tshs 2,000/= kwa siku.
3. Magari madogo (Teksi/gari binafsi) Tshs 500/= kwa siku.
4. Ushuru wa choo kila anayepata huduma Tshs 300/= kwa huduma.
5. Wafanyabiashara ndogondogo ndani ya stendi Tshs 200/= kwa siku.
6. Kila mfanyabiashara ndani ya stendi ahakikishe kuwa anakihifadhi taka (dust bin) kwa ajili ya kuhifadhi taka, ukibainika hauna utatozwa faini isiyopungua Tshs 50,000/= na kuendelea.
7. Kulaza magari katika stendi ya zamani itakuwa ni Tshs 3,000/= kwa siku.
NB: 1. USHURU WA MAGARI YA STENDI YATAENDELEA KULIPA KAMA KAWAIDA.
TOZO HIZI NI KWA MUJIBU WA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA
MBULU
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.