Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mheshimiwa Joseph Mandoo amewataka madiwani na wakuu wa idara wote kushirikiana ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shule kabla ya muda uliopangwa kuisha.
Hayo yamesemwa wakati akifungua baraza la madiwani robo ya pili ya Octoba-Desemba 2024/2025 ambapo amesea kuwa serikali inatumia fedha nyingi kujenga mashule lakini mwisho wa siku vyumba vinakua tupu au wanafunzi wachache kitu ambacho sio sawa na tunarudisha nyuma juhudi za Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan.
“Wanafunzi wote waliofaulu Kwenda kidato cha kwanza wahimizwe Kwenda shule kwa kushirikiana maafisa elimu pamoja na watendaji kata na vijiji.”alisema Mheshimiwa Mandoo.
Pia Mh Mandoo alisema kuna umuhimu wa kujitathimini kwanini shule zetu za msingi bado hazifanyi vizuri sana,hivyo mikakati lazima ifanyike ili ufaulu uongezeke.Pia alisema kuwe na utaratibu wa kupongeza walimu na shule zinazofanya vizuri ili kuleta motisha kwa wengine nao wafanye vizuri,lakini pia inaleta hari kuwa wametambulika na kufanya waendelee kufanya vizuri.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu ndugu Abubakari Kuuli alisema uandikishaji wa wanafunzi wa elimu msingi na uripotiji wa wanafunzi wa sekondari bado hauridhishi licha ya kuwashirikisha watendaji kata kwenye zoezi.Hadi sasa ni asilimia 51 za wanafunzi wa elimu msingi ndio wameandikishwa na asimilia 52 ndio wameripoti shule kwa upande wa sekondari.
Pia Mkurugenzi alitoa ripoti ya ufaulu kwa matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2024 na kusema kuwas ufaulu umefika asilimia 98.7 ambapo umeongezeka kwa asilimia 3.7 kutoka matokeo ya mwaka 2023.
Pia alisema kama halmashauri wanamkakati wa kuunda kamati ambayo waheshimiwa madiwani watakwep ndani yake kukaa na shule zilizofanya vizuri na zile ambazo hazijafanya vizuri ili kujua changamoto ni nini mpaka inapelekea shule nyingine zinafanya vizuri na nyingine hazifanyi vizuri.pia kwa shule ambazo zitakua zimefanya vizuri zitapewa zawadi na zile ambazo zitafanya vibaya watawajibika.
Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Mbulu Paulo Bura alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu kuhakikisha shule ya sekondari Eshkesh wanafunzi wanaripoti haraka iwezekanavyo.Pia alisema japo serikali imetoa muda wa wanafunzi kuripoti shule hadi March 31 lakini mwanafunzi atakaye ripoti January na atakayeripoti March hawawezi kuwa sawa darasani.Hivyo wazazi wahimizwe wapeleke wanafunzi mapema hata kama hawana sare.
Naye mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Mbulu ndugu, aliwashukuru viongozi wote kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya na kuwaomba shule za sekondari za kidato cha 5 na 6 ziongezwe kwani halmashauri hii ni kubwa na shule zilizopo ni mbili tu,kwa kuongeza shule hizi kunaleta ufaulu kuongezeka kwani wanafunzi wa madarasa ya chini nao watatamani kufika walipo wenzao.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.