Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mbulu limeipongeza serikali kwa kusimamia maamuzi ya ujenzi wa Makao Makuu kuwa Dongobesh kutokana na mapendekezo ya baraza na hata baada ya ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara iliyofanyika tarehe 04-09/03/2018 ambapo alishauri kuwa ujenzi ufanyike Haydom na kuwaagiza Mwenyekiti na Mkurugenzi kuitisha baraza maalum ili kujadili maoni hayo.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa ukumbini kuendelea na mjadala wa kikao.
Akiongea kwenye kikao hicho kilichofanyika hii leo tarehe 25/04/2018, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph Mandoo amewaomba Waheshimiwa madiwani kutumia kikao hicho kuweza kupanga na kusimamia maendeleo ya Halmashauri kwa ujumla.
“Napenda kutumia fursa hii kuipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Joseph Magufuli na Uongozi wake kwa ujumla kwa kuwa makini na kusimamia kile kinachotekelezwa kwa umakini na Watendaji wake wa chini wanachokipanga na kukipitisha ili kuleta maendeleo kwa wananchi”, amesema Mhe. Mandoo kwenye kikao cha baraza hilo.
Mhe. Joseph G. Mandoo Mwenyekiti wa Halmashauri akisoma kwa makini muhtasari unaowasilishwa
Kufutia vikao vya Kisheria vilivyokaa kwa ngazi tofauti vya maamuzi, uongozi ulipokea rasmi barua ilikielekeza ujenzi huo ufanyike katika Mji wa Dongobesh kama ilivyokuwa mapendekezo ya Baraza la Waheshimiwa Madiwani. Mhe. Mandoo ametoa ufafanuzi wa kina kuwa taratibu zote za kisheria zimezingatiwa na taratibu za kuthamini mali na ardhi pia zimefuatwa na hivyo kuomba taratibu za ujenzi kuanza mara moja katika eneo husika.
Kaimu Mkurugenzi Ndugu Michael Faraay akipitia baadhi ya nyaraka zinazowasilishwa na kamati mbalimbali
Akitoa maagizo ya Serikali juu ya ujenzi huu wa makao makuu, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Chelistino Mofuga ameshauri baraza la Madiwani kupitia Mwanasheria wa Halmashauri waweze kuzingatia taratibu zote za kimikataba kwa wananchi waliotoa ardhi yao ipatayo hekta 102.
Mhe. Chelestino Mofuga Mkuu wa Wilaya ya Mbulu akiwa katika kikao cha baraza akisoma kwa makini taarifa inayowasilishwa
Aidha Mhe. Mofuga ametumia fursa hiyo kukemea vikali taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao kuhusu maandamano na kuliagiza jeshi la Polisi kuanza doria mara moja, na kutoa onyo kali kwa watumishi watakaobainika kujihusisha na kuhamasisha maandamano hayo hatua kali zitachukuliwa juu yao.
baadhi ya Wataalam waliohudhuria kikao, kutoka kulia ni Afisa Mipango, Mweka hazina na Afisa Utumishi
Akihitimisha kikao hicho cha baraza, Mwenyekiti wa halmashauri awaomba wataalam kusimamia na kutekeleza ipasavyo maagizo waliyotoa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.