DONGOBESH-MBULU ��� OCT 1, 2023
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, Amempongeza na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mheshimiwa Flatei Massay kwa kazi kubwa na nzuri anayo ifanya ya kuinua michezo katika jimbo lake.
Komred Kheri James ameyasema hayo mapema leo katika zoezi la ufunguzi wa mashindano ya Flatei Jimbo Cup, yanayo shindanisha vijana wa kata zote za jimbo la Mbulu Vijijini katika mchezo wa Kabumbu.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo, Komred Kheri James ameeleza kuwa michezo ni Afya, Ajira, Burudani na nyenzo muhimu ya kujenga umoja na mshikamano wa jamii. Hivyo Serikali itaendelea kuunga mkono michezo yote na itaendelea kushirikiana na wadau katika kujenga miundombinu, kuongeza Wataalamu wa michezo na kupanua wigo wa fursa za kimichezo ili vijana waweze kunufaika na fursa za ndani pamoja na nje ya Nchi.
Pamoja na mambo mengine, Komred Kheri James amesema atamuunga mkono Mheshimiwa Mbunge kwa kuongeza zawadi ili kuchochea ushindani katika mashindano hayo.
Flatei Jimbo Cup ni mashindano ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa ufadhili wa Mheshimiwa Mbunge na yametumika vyema katika kuibua vipaji, kulea vipaji na kuendeleza vipaji vya Kabumbu katika jimbo la Mbulu Vijijini na Wilaya nzima kwa ujumla.
#Kwa pamoja. Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.