Akifungua Kikao kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama(W),Wataalamu na Wadau mbaliimbali wa maendeleo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya maandalizi ya utoaji chanjo kwa watoto kuanzia miezi 9 hadi chini ya miaka 05 yanayotarajiwa kufanyika tarehe 15-18/02/2024, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Lazaro Twange ambaye anakaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.
Mhe. Lazaro Twange akiongea wakati wa kufungua kikao hicho amewataka kila halmashauri zote kuhakikisha wanafanya maandalizi yakutosha ya utoajichanjo kwa njia mbalimbali ili kuwezesha kila mwananchi aliye na mtoto wa umri huo anapata chanjo.
“Sitegemei kusikia katika halmshauri zangu kuna mwananchi analalalimika kutopata chanjo au kusikia kuna kifo cha mtoto kinatokea kwa kusababishwa na maradhi ya Surua Rubella”alisema DC Lazaro Twange
Wakichangia kwa nyakati mbalimbali Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Mbulu mji wameeleza ni kwa jinsi gani wamejiandaa kuwafikia watoto katika maeneo yote ya halmashauri husika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya,
“Mhe. Mkuu wa Wilaya tupende kukuhakishia kuwa kupitia viongozi wetu wa ngazi mbalimbali kama vile balozi, mtendaji wa mtaa, kitongoji, kijiji, kata, Maafisa Elimu kata na Wakuu wa shule tutahakikisha tunawafikia walengwa kwa namna moja au nyingine”, walisema hayo Wakurugenzi.
Mkuu wa Wilaya amawaomba Wenyeviti wa halmashauri kupitia Mabaraza ya Madiwani wanahakikisha Waheshimiwa wote wanasimamia kwa uangalifu zoezi hili katika kata zao ili wananchi waweze kupeleka watoto kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya amehitimisha kwa kuwahasa wananchi kuwa huduma itatolewa bure kwa maeneo ya vituo vya huduma za Afya na sehemu mbalimbali zilizotengwa.
#KwaPamoja, Tunaijenga Mbulu Yetu
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.