Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya mama huadhimishwa Duniani kote tarehe 1-7 Agosti kila mwaka. Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya mama Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1992 ikiwa na kaulimbiu za kila mwaka zikigusia mifumo ya afya, Kanuni za Kimataifa za Uuzaji na Usambazaji wa maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo, usaidizi wa jamii, ikolojia, uchumi, sayansi, wanawake na kazi, pamoja na elimu na haki za binadamu. Tangu mwaka 2016, Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya mama Duniani imekuwa ikiendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals) yanayojumuisha kiashiria cha “Unyonyeshaji Watoto maziwa ya Mama pekee” ili kuhakikisha kuwa suala la unyonyeshaji linapewa nafasi katika mpango wa maendeleo katika sekta ya afya na lishe Duniani. Mnamo mwaka 2018, Baraza la Afya Duniani (WHA) liliidhinisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya mama Duniani kama mkakati muhimu wa kukuza unyonyeshaji.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.