Kikao cha baraza la madiwani limefanyikwa kwa mara ya kwanza hii leo tarehe 8/11/2019 katika mji wa Dongobesh ikiwa ni kikao cha kawaida kujadili taarifa mbalimbali za Kamati za kudumu za halmashauri kama vile elimu,Afya, Uchumi, fedha na Mipango, Huduma za jamii na kadhalika hii ni mara tu tangu kuhama kwa Makao Makuu katika Mji wa Dongobesh toka tarehe 30/10/2019 kutokana na tamko la Mhe. Waziri wa Tamisemi kuzitaka Halmashauri 81 nchini kuhamia Makao Makuu ya halmashauri husika.
Muonekano wa ndani wa Kikao cha Baraza katika Soko la wazi la Dongobesh maeneo ya Stendi.
Akifungua kikao hicho cha baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Joseph G.Mandoo amelipongeza baraza la Madiwani kwa ujumla pamoja na timu nzima ya Wataalam kwa kuridhia kuhamisha Makao Makuu katika Mji wa Dongobesh na kusogeza huduma karibu na Wananchi.
Aidha amewaomba wananchi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Dongobesh na nje ya Dongobesh kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza ikiwa ni pamoja na kuchukua Viwanja vitakavyogawiwa kwa wananchi wote bila upendeleo.
Akitoa salamu za Serikali Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi. Sara amelipongeza Baraza la Madiwani na Wataalam kukubali kufanyia Dongobesh hata pasipokuwa na eneo la Mikutano nah ii ni kuonesha jinsi gani uongozi unapokea maagizo mbalimbali yanayotolewa na Serikali.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. Saraha akipitia kabulasha linalowasilishwa wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani katika Mji wa Dongobesh
Bi. Sara ameendelea kusema kuwa Serikali imejipanga kuboresha Mji wa Dongobesh na kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha zimetengwa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa km.50 kutoka Mbulu kupitia Dongobesh mpaka Haydom hii ni kuonesha jinsi gani Serikali ya awamu ya tano iko karibu na wananchi kwa kuwahudumia zaidi.
Ndugu Hudson S. Kamoga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akiwa katika Kikao cha Baraza
Akiongea katika Kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji ndugu Hudson S.Kamoga amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kuendelea kuonesha ushirikiano wa dhati kwa Wataalam na kuzidi kuwaomba kushirikiana zaidi hasa kwa kuwatumika kwa karibu zaidi.
Ndugu Kamoga ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa ni jinsi gani imehamua kuleta maendeleo makubwa zaidi kwa Wananchi wa Mji wa Dongobesh kwani Serikali imewekeza miradi mikubwa yenye thamani ya fedha nyingi za wananchi kama vile Ujenzi wa Makao Makuu, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ukarabati na Uboreshaji wa huduma za Jamii katika Kituo cha Afya Dongobesh, Ujenzi Mkubwa wa bwawa la Umwagiliaji, Ujenzi wa barabara ya lami kwa urefu wa Km.1 na maendeleo mbalimbali.
Mhe. Flatei Massay akichangia jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani liliofanyika katika mji wa Dongobesh
Akichangia katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay amewahidi kuendelea kuonesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kufuatilia ahadi zote zilizokwisha kuhaidiwa na Mawaziri mbalimbali waliokwisha pita katika jimbo hilo kwa mfano ukamilishaji wa Ujenzi la Utawala, ahadi za maji sehemu mbalimbali na amelihakikishia baraza hilo baadhi ya vijiji visivyokuwa na umeme utawaka karibuni.
Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa kamati ya fedha Mhe. Joseph Barabojick(Diwani kata ya Dongobesh -CCM) akiwasilisha taarifa ya kamati yake mbele ya Wajumbe wa Baraza
Mhe. Ester Joel Mwenyekiti Kamati ya Uchumi na Diwani Viti Maalum kata ya Dongobesh(CCM) akiwasilisha taarifa ya kamati yake
Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii Mhe. Joseph Tsaxaitu na Diwani wa Kata ya Masieda (CCM) akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na Wajumbe
Katika kikao hicho cha Baraza kiliweza kujadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo kutokana na jinsi Kamati zilivyowasilisha na kujadiliwa, aidha Baraza limeridhia kukabidhi Jengo lililokuwa la Utawala kwa Halmashauri ya Mji kwa hati ya makubaliano,kwani kutokana na mgawanyo wa Mali na Madeni Jengo hilo la Halmashauri lilikuwa ni mali halali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Ndugu Horace Kolimba Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ikilieeza Baraza jinsi hatua gani zitatumika katika kukabidhi jengo la Utawala
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani
Timu mbalimbali za Wataalamu wakiwa ukumbini kufuatilia Mada mbalimbali zinazochangiwa na Wajumbe.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.