Mgeni Rasmi Mhe.Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (Mb) Akiongea Katika Kiwanja cha Mpira cha CCM Kata ya Dongobesh - Mbulu
Timu ya Saumu Football Club Wakati Inajiandaa Kuingia Uwanjani.
Timu ya Saumu Football Club Wakiwa kwene Mpambano Mkali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A.A.Kuuli Akisalimia Wananchi.
Mh.Diwani Viti Maalumu Toka Kata ya Dinamu Akisalimia Wananchi na Kulia ni Mh.Mbunge Flatei wa Jimbo la Mbulu Vijijini.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota Akisalimia Katika Fainali hizo
Kijana Aitwaye Silviani Dionis Ndiye Aliyepewa Zawadi ya Mchezaji Mwenye Magori Mengi Jumla ya Magoli 21 Kutoka Timu Yake ya Saumu FC Toka Kata ya Bashay
Timu ya SAUMU FC (BASHAY) Wakikabidhiwa Kombe Hilo na Mhe.Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (Mb) Kulia ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Leo tarehe 14.11.2021
~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo ambapo fainali za Kombe la Mh. Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei kukamilika salama na washindi kukabidhiwa kombe za zawadi zingine kemkem. Michezo hii ilianza kutimua vumbi tangu tarehe 03.10.2021 katika kiwanja cha CCM kata ya Dongobesh - Mbulu, kwa kushirikisha timu 29 toka kata zote za jimbo la Mbulu Vijijini. Katika fainali hizi mwisho wake zilibaki timu 8 ambazo ziliingia robo fainali nazo ni Dongobesh FC toka Kata ya Dongobesh, Mang'nay FC toka kata ya Bashay, Jogoo FC kata ya Gidhim, Jambina FC kata ya Dongobesh, NOWU FC toka kata ya Tumati, Qatajirig Tumati Saumu FC Bashay na WAIS Tango toka kata ya Tumati.
Nusu fainali ilichezwa tarehe 12.11.2021 kati ya Dongobesh FC 0 na Saumu FC 1 kisha tarehe 16.11.2021 Jambina 0 na NOWU 2 na katika kutafuta mshindi wa tatu ikabidi Dongobesh FC wapambane vilivyo na Jambida ambapo matokeo ilikuwa Dongobesh 1 na Jambida 0. Na hatimaye fainali ya leo kukutana uso kwa uso kati ya Saumu FC na NOWU FC ambapo refarii alikuwa Bw. Ahmed Arajiga wa Haydom
Kijana aliyeshambulia nyavu zote dhidi ya NOWU na kusabibisha majanga kwao ni Silviani Dionis ambaye hata kimagoli peke yake hadi mechi zilipoisha leo alikuwa na jumla ya magoli 21 kutoka timu yake ya Saumu FC toka Kata ya Bashay na yeye ndiyo mchezaji aliyechukua zawadi ya kufunga magoli mengi katika michezo hii ya Mh. Mbunge Flatei. Baada ya ushindi huu zawadi zilitolewa kwa washiriki mbalimbali walioonyesha vipaji vyao zaidi ya wenzao. Timu ya Saumu iliyochukua kombe imekabidhiwa zawadi ya set 1 ya jezi, mpira 1 na fedha taslimu Tsh. 500,000/= Timu ya pili ilikuwa NOWU hii ilipewa zawadi ya set 1 ya jezi, mpira 1 na fedha taslimu Tsh. 400,000/= huku timu ya tatu ilikuwa ni Dongobesh FC ambayo ilipewa zawadi ya mpira 1 na fedha taslimu Tsh. 100,000/=
Hata hivyo zawadi zingine zilikwa za Mchezaji bora ambaye alkuwa ni Paulo Paskali toka timu ya Dongobesh FC kata ya Dongobesh ambaye alipewa jezi 1, golikipa bora alikuwa ni JacobJohn toka timu ya Saumu Kata ya Bashay. Katika fainali hizi Mh. Gekul aliongozana na mwenyeji wake Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria V. Makota, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. A.A.Kuuli na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Mh.Mbunge Flatei mwenyewe.
Michezo hii ni muhimu sana katika kushajiisha uchumi wa kiwilaya kupanda kwa kusaidia mzunguko wa kifedha kwa mnyumbuliko wa wananchi mbalimbali wanaoshiriki katika mnyororo wa shuguli zote za michezo hii kuanzia ajira na kipato katika usafirishaji, chakula, malazi na mahitaji mengine muhimu huku uendelezaji na ukuzaji wa vipaji vya vijana katika tasnia nzima ya michezo ikikua. Mh. Mbunge Flatei ni mwanasiasa mwenye juhudi ya kazi, mtazamo chanya na wa kimamboleo katika kila nyanja ya maendeleo katika jimbo la Mbulu Vijijini kwa maslahi mapana ya wanachi wa Mbulu na Taifa kwa ujumla.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.