Serikali kupitia Baraza la Mtihani la Tanzania limetangaza muundo mpya wa Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Akitanganza Muundo huu mpya leo tarehe 20/03/2018,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania amesema muundo huu wa utungaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi(PSLE) utaanza mwaka huu 2018.
Mabadiliko hayo ameyatangaza wakati anawasilisha mada ya “TATHIMINI YA UFAULU WA SHULE ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKALI”katika mkutano mkuu wa tano wa Maafisa Elimu Mkoa na Wilaya uliofanyika Dodoma.
Aidha akitoa rai kwa Walimu wa Wakuu wa shule za msingi amesema ni matarajio ya Serikali kuwaona Walimu hao wakianza kuwapima wanafunzi katika mitihani mbalimbali kwa kutumia muundo uliotolewa na baraza ili kuwajengea uzoefu mapema.
“Tunaomba upimaji uzingatie ngazi zote kuanzia ngazi ya shule, kata na kanda”amesema Katibu Mtendaji.
Bonya hapa kupata muundo huu:- FOMATI YA PSLE FEB 2018.pdf
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.