Aliyesimama ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Katika Zoezi la Uhamasishaji Chanjo ya UVIKO 19.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, S. Sanga Akiwa Katika Zoezi la Uhamasishaji Chanjo ya UVIKO 19
Katikati ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota.
Aliyesimama ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Shirima Katika Zoezi la Uhamasishaji Chanjo ya UVIKO 19.
Wataalamu wa Afya Wakiendelea na Kazi Iliyowaleta, Ni mwendo wa Kuchanja tu Kama Unavyojionea kwa Hawa Wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Maretadu Wakisikiliza Wataalamu Wanavyowaelimisha Juu ya Chanjo ya UVIKO 19
~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~
Katika hali ya kuhakikisha wananchi wanaendelea kufanya kazi zao vizuri za kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi hatimaye kuwa salama na gonjwa hatari la UVIKO 19 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ahamasisha kwa nguvu zote wananchi kijiji kwa kijiji, kata kwa kata ili tu elimu itolewe itakayopelekea wananchi kuwa na mwamko wa kuchanja UVIKO 19 bila shida.
Katika utoaji wa elimu hiyo Mh. Mkuu wa Wilaya, S. Makota aliungana na wataalamau wa afya ngazi ya Wilaya ambao nao walikuwa wamejipanga ipasavyo kutoa elimu ya UVIKO 19, chanjo ya UVIKO 19 na utoaji wa chanjo husika kwa wanaohitaji. Katika Kijijiji cha Maretadu na viunga vyake wananchi walijitokeza wengi katika kupata elimu hiyo iliyopelekea watu takribani 50 kuchanjwa chanjo ya UVIKO 19 jambo lililosisimua sana watu.
Wataalamu wa afya waliendelea kusisitiza kwamba hakuna madhara wakati na baada ya kuchanja kama inavyosemkekana na wengi kwasababu kitu cha kwanza kabisa hutaweza kuambukizwa tena na UVIKO 19 kwani kinga zitakuwa zimeimarika sana, na hata ikitokea ukaugua kiwango cha kuathirika aliyechanjwa huwa kidogo au hakuna kabisa wakati huo huo asiyechanjwa akiambukizwa hutumia gharama kubwa sana katika kujitibu ambapo kwa utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya imejulikana kwamba ni kati ya Tsh. 200,000/= hadi Tsh. 300,000/= kwa mtu moja kwa siku, hizi ni gharama za kuokoa uhai wa mgonjwa wa UVIKO 19, hivyo wananchi wanatakiwa kufanya juu chini kuchanja tu ndiyo kinga pekee kwani hakuna dawa ila watabibu wote hutibu dalili inayojitokeza kwa mgojwa tu, mfano kama anaharisha atatibiwa kuhara ili asiendelee kuharisha.
60% ya wananchi wanaopaswa kuchanja watachanjwa na zoezi hili ni endelevu, hata hivyo imefahamika kwamba vituo vya kuchanjia ni sehemu zote za kutolea huduma ya afya kuanzia Zahanati, Vituo vya afya na Hospitali zote za Wilayani.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.