Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu. Hudson S. Kamoga ametoa ufafanuzi juu ya Ujenzi wa Makao Makuu, akitoa taarifa baada ya kupokea maelekezo ya Serikali amesema kuwa Serikali imeagiza halmashauri kujengwa katika mji wa Haydom na hii ni kutokana na sababu mbalimbali.
Muunekano wa jengo la zamani la halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Akikiri kupokea fedha kiasi cha shilingi bilioni Moja na Milioni Hamsini ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa awali wa jengo hilo, ameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Magufuli kwa kuonesha juhudi za kosogeza huduma kwa wananchi kwani wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufika makao makuu,na kuhaidi kusimamia kikamilifu ujenzi huo na ikiwezekana ifikapo mwezi Machi au Aprili 2019 ujenzi uwe umekamilika na hatimaye kuhamia rasmi.
“Serikali ya awamu ya tano kupitia bageti ijayo ya mwaka wa fedha 2018/2019 imetenga kiasi cha Bil. 2.3 ambazo zinazotarajiwa kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kukamilisha ujenzi huo”amesema Mkurugenzi Kamoga.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.