Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli, Katibu wa Afya Wilaya ya Mbulu na Mwisho ni Afisa Lishe (W) Ndg. Ally Fupi .
Aliyesimama ni Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Ally Fupi .
Wajumbe wa Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~
Katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji shughuli za lishe kwa kipindi cha julai 2021 - juni 2022
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imefahamika kwamba ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 30, kati ya hizo vituo 25 vinavyotoa huduma za kliniki ya uzazi na mtoto pia kuna jumla ya kliniki mkoba na tembezi 33. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 halmashauri kupitia Idara ya afya imetekeleza shughuli mbalimbali za lishe kama vile kufanya uhamasishaji na kutoa elimu juu ya lishe bora ngazi ya jamii kwenye kata 13, kutoa matone ya vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka 5 watoto 51,173 sawa na 104% ya waliopata matone ya Vitamini. “A”.
Tulipokea chakula dawa kutoka bohari kuu ya dawa ya Taifa “MSD” na Mkoani, makasha 18 yenye ujazo wa P/150. Makobo 48 ya maziwa (F75) kutoka bohari kuu ya dawa ya Taifa “MSD” kwa ajili ya watoto wenye utapia mlo. Katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama na hali ya utapiamlo, idara ya afya iligawa chakula dawa na maziwa ya kopo kwa watoto 14 waliokuwa na utapia mlo mkali na watoto 73 walio kuwa na utapia mlo wa wastani. Ili mama awe na uzazi bora anahitaji madini ya chuma ambapo kwa akina mama wajawazito 43,521 sawa na 92.3% walipata madini ya chuma kati ya akina mama 40,211 walio hudhuria kliniki ya uzazi na mtoto.
Kwa idara ya afya kitengo cha lishe kuna changamoto kadhaa ambazo tunaedelea kuzitatua kwa kushirikiana na jamii husika kama vile; Uelewa mdogo juu ya lishe bora kwa jamii, muitikio mdogo kwa wanaume kupeleka wake zao kliniki pamoja na kupata elimu ya uzazi. Pia baadhi ya akina mama huchelewa kuanza kliniki ndani ya wiki 12 na wengine kujifungulia majumbani na mwisho ni suala la akina mama kutokuzingatia uzazi wa mpango kwani huzaa watoto kwa muda mfupi chini ya miaka miwili.
Kwa kuwa wataalamu wapo na nyenzo zingine za kufanyia kazi tutaendelea kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa jamii ngazi ya kata na vijiji juu ya lishe bora na umuhimu wa kuanza kliniki ya uzazi wa mama na mtoto mapema zaidi kwa mwaka wa fedha 2022-2023. Kufanya mafunzo msasa kwa watumishi ngazi mbalimbali ili kuwa na uelewa msawazo katika ngazi zote. Katika sekta ya elimu tutaendelea kutembelea na kutoa elimu juu ya lishe mashuleni Msingi na Sekondari ikiwa ni pamoja na kuunda klabu za lishe 20 na kuziimarisha klabu zilizopo mashuleni.
Ili kuwa na lishe bora uwepo wa chakula pekee hakukidhi haja bali kwani mapishi stahiki ni suluhisho la kupata virutubisho vyenye kiwango cha juu hivyo kuwepo kwa mafunzo darasa “cooking class demonstration” kila robo mwaka ngazi ya jamii katika kata 4 litafanyika. Halmashauri itaendelea kuongeza fedha za lishe kupitia idara na vitengo vilivyopo ili kuzifanya shughuli za lishe kuwa zenye tija zaidi na endelevu kwa jamii.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.