Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akishirikiana na Wanakijiji cha Dongobesh kupanda miti 2800 ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akipanda Miti hiyo leo tarehe 25/03/2020 katika eneo la Bwawa la Umwagiliaji maeneo ya Dongobesh.
Tunachapa kazi na kuzingatia tahadhali zote juu ya CoronaVirus. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga(mwenye kofia) na Mratibu wa Mradi wa MVIWATA Donald Laizer.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakishirikiana na Wadau mbalimbali wamepanda miti mbalimbali na hasa miti asilia inayokwenda sambamba na hali ya hewa ya Wilaya hiyo.
“Tumeshajiwekea Mkakati na Kampeni ya Kupanda Miti zaidi ya 5000 katika maeneo yote halmashauri ya Mbulu yenye vilima na miiniko iliyowazi ili kuweka urithi bora wa kizazi cha sasa na baadae” alisema Hudson Kamoga.
Pamoja na Upandaji wa Miti ya Mbao,pia alisisistiza wananchi kuandaa na Kupanda miti ya Matunda,iadha zoezi hilo lilifanyika akiwa akiwa na Mratibu wa MVIWATA Manyara ndugu Donald Laizer na amashukuru Mkurugenzi kwa ushirikiano anaoupata na kuhaidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika uboreshaji wa Mazingira.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.