Mbulu.
Na mwandishi wetu
Baraza la madiwani Halamshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani manyara leo 09.03.2018 limepitisha ujenzi wa makao makuu ya halamshauri ya Wilaya hiyo kujengwa Dongobesh tofauti na mapendekezo ya Mkuu wa mkoa wa Manyara ya kujengwa Haydom.
Wajumbe wa Baraza Maalum la Madiwani wakisoma kwa makini mada inayowasilishwa.
Hayo yamejiri katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kikao maalumu kilichoitishwa kwa ajili ya kujadili Agenda kuu mbili ambazo ni eneo la kujenga makao makuu ya halmashauri nay a pili ni kujadili maombi ya mwekezaji kijiji cha Eshkesh Wilayani Mbulu.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Joseph Mandoo , aliomba muongozo wa kisheria ili kutoa maamuzi baada ya baraza kujadila kwa muda mrefu na hatimaye ikaamuliwa kupigwa kura ya siri ili kuamua ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Timu ya wataalam wa Halmashauri ikifuatilia mjadala ukumbini
Madiwani waliopiga kura jumala walikuwa 23 na kura halali zilizopigwa zilikuwa 23, kati ya kura hizo(17) zimependekezwa Makao Makuu kujengwa dongobesh na kura (6) walipendekeza ujenzi uwe Haydom.
Awali akitoa maelezo kwanini makao makuu yajengwe Haydom mkuu wa wilaya ya Mbulu bwana Chelestino Mofuga amesema Haydom miundo mbinu yake iko vizuri lakini madiwani kwa upande wao wamesisitiza kuwa yajengwe Dongobesh kwa kupitia michango mbalimbali waliyoitoa na hatimaye kura kuamua.
Meza kuu ikisikiliza maoni toka kwa wajumbe wa baraza.
Hayo yamejiri baada ya mkuu wa mkoa wa manyara Bwana Alexanda Mnyeti kufanya ziara Wilayani humo na kupendekeza makao makuu ya halmashauri ya wilaya yajengea Haydom nakuwataka madiwani kujadili upya mchakato huo na kutoa mapendekezo.
Katibu wa kikao na mwanasheria wakishauriana jambo
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.