Tumewaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala lakini kukawa na mivutano ya wapi pangefaa kuwa Makao Makuu ya Wilayah ii ambapo ndipo Jengo hili lilitakiwa kujengwa: Ninachofurahi kuona leo ni kuwa mlipokea maelekezo na jengo limejengwa katika eneo la Dongobesh ambapo ni katikati ya Wilayah ii na rahisi kwa wananchi kufika kutoka kila pande za Wilaya hii”Alisema Jafo.
Muonekano wa Jengo jipya la Utawala halmshauri ya Wilaya ya Mbulu Ukiendelea
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Manyara na kutembelea ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mbulu linalojengwa katika eneo la Dongobeshi.
Kwa kujenga jengo hili Dongobesh mmewatendea haki Wananchi wa Mbulu kwa kuwa mmewapunguzia gharama ya muda na umbali ambao kwa muda mrefu imewagharimu kufuata huduma za Muhimu katika Ofisi za Serikali aliongeza Jafo.
“Nimeridhishwa na ujenzi unaoendelea na nimefurahi kuona mmeshakamilisha majengo ya chini, nimeridhishwa na ubora wa Jengo pamoja na gharama nafuu toka kwa Mkandarasi Mzinga holding Company pamoja na Mhandisi Mshauri Dar es salaam Institute of Technology (DIT) niseme kazi nzuri na hongerni sana ” alimalizia Jafo.
Akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hudson Kamoga amesema ujenzi wa jengo la Utawala unafanyika kwa awamu tatu na katika awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa jengo la mbele ambalo litagharimu tsh Bil 4.7 awamu ya pili itahusisha ujenzi wa ukumbi, ghala na mgahawa na awamu ya tatu utahusisha ujenzi wa pande mbili za nyuma ya jengo.
Kamoga aliongeza kuwa Jengo hilo la Utawala limekadiriwa kujengwa kwa gharama ya Tsh 6.7 ambapo gharama za ujenzi ni Bil 6.3 na gharama sa mhandisi mshauri ni mil 351 huku gharama sa kuandaa mchoro zikigharimu tsh mil 30 tu.
Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Mbulu umetokana na kugawanyika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupatikana kwa Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupelekea Mbulu Mji kubakia Mjini na Halmashauri ya Wilaya kuhamia katika eneo la Dongobesh ambapo ujenzi huo unaendelea.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.