Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndug Hudson Kamoga ameongoza mamia ya watumishi walioojitokeza kuuadhimsha sherehe za Mei Mosi Wilayani mbulu zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Haydom na kupambwa na maonesho mbalimbali toka makundi tofauti tofauti kama yalivyoandaliwa.
mamia ya wananchi na watumishi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya shule ya msingi Haydom
amewataka watumishi kutokuwa waoga katika kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kueweza kuepukana na magonjwa nyemelezi. Akiwakumbusha kufanya mazoezi kila jumamosi sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi, watumishi wajenge mazoea yakufanya mazoezi.
“nikuagize Mganga Mkuu kupitia mashindano ya mchezo wa mpira yanayoandaliwa na Mkurugenzi yatakayofanyika hapa haydom kuanzia tarehe 13-20/05/2018 hakikisha kunakuwa na banda la kupima afya ili kutoa fursa kwa vijana wetu watakaoshiriki mashindano hayo kupima na kujua hali ya afya zao” alisema Kamoga.
kikundi cha kwaya toka chama cha Walimu kikitoa burudani viwanjani hapo
Aidha akiongea mbele ya Watumishi waliojitokeza katika Viwanja hivyo Mkurugenzi Mtendaji amewakumbusha watumishi kuwa wabunifu na kuonesha ufanisi zaidi katika maeneo yao ya kazi ili kutoa huduma inayostahili pale mwananchi anapokuwa akihitaji huduma na sio kukaa na kusubiri sherehe za mei mosi kuja kupokea zawadi pasipo kuonesha uhodari wako katika eneo lako la kazi.
watumishi mbalimbali waliojitokeza wakiendelea kufurahia maonesho viwanjani hapo
Wakitoa salamu za pongezi wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi wameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa watumishi na kuiomba serikali kutatua changamoto zinazowakabili watumishi na kuhaidi kumpatia ushirikiano wa kutosha Mkurugenzi kila anapohitaji kutoka kwao.
mmoja ya wafanyakazi hodari akipokea zawadi toka kwa mgeni rasmi
Aidha mgeni rasmi katika sherehe hizo katibu Tawala Msaidizi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ndugu kaogo amewataka watumishi kuendelea kushikamana na kuchapa kazi kwa bidii na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele kwa kuonesha uzalendo na sio kukuaa vijiweni na kuilalamikia Serikali pasipo kuonesha ufanisi wa kazi zao.
mgeni rasmi ndugu Kaogo akiongea na wafanyakazi waliopo kwenye viwanja hivyo
Kaogo amesema serikali ya awamu ya tano iko makini na inaendelea kutatua changamoto zote zinazokuwa zinawakabili watumishi na kuaidi kutoa ushirikiano kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya pale watumishi wanapokuwa wanahitaji kupewa msaada wowote.
wafanyakazi mbalimbali wakifurahia maonesho yanayoendelea viwanjani hapo
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.