���TLAWI - MBULU ��� NOV 12, 2023
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James mapema leo, ameipokea Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliowasili wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji Tlawi.
Akizungumza na Wananchi katika Kata ya Tlawi Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Daniel Sillo, ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa sana na kasi ya utekelezaji wa mradi huo ambayo pia imejali viwango vya ubora na thamani ya fedha. Mheshimiwa Sillo ameipongeza Wizara ya Kilimo, Tume ya Umwagiliaji na Uongozi wa Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Mbulu kwa usimamizi na ufatiliaji wa karibu wa mradi huo muhimu na wakimkakati kwa faida ya Wananchi.
Mradi wa Umwagiliaji - Tlawi unajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni sita na Milioni mia nne, na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu. Mradi huu utakapo kamilika unatarajia kuleta manufaa kwa Wananchi wapatao 2400 wanaoishi katika vijiji vya Tlawi, Gunineda, Jaranjar, Baidosla na Gendi.
Pamoja na faida zingine za mradi huu, Wananchi wataweza kulima kwa msimu zaidi ya mmoja, Wataepukana na kilimo cha kutegemea mvua, na kiwango cha Mavuno kitaongezeka na biashara ya mazao ya kimkakati kama kitunguu Swaumu itaimarika.
Akiwasilisha salamu za Serikali katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga ameipongeza Kamati kwa ziara hiyo muhimu, ameeleza dhamira na mikakati ya Serikali ya kuendelea kuibua na kusimamia miradi yote ya kisekta katika mkoa, na ameishauri Wizara ya Kilimo kuangalia upya utaratibu wa kudhibiti bei ya pembejeo ili mkulima alioko kijijini asiumizwe na tamaa za wasambazaji wasiokuwa waaminifu.
Ziara hii pia Imehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani, Mbunge wa viti maalumu, Viongozi, Watumishi na Wananchi wa kijiji cha Tlawi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji.
Kamati ya Bunge imekamilisha salama ziara yake ya siku moja Wilayani Mbulu, na imewashukuru na kuwapongeza viongozi na Wananchi wa Mbulu kwa ukarimu na makaribisho mema.
#Kwapamoja, Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.