Na Ruth Kyelula, Mbulu - DC
Mwenyekiti wa Halmashauri Joseph Mandoo, ametoa wito kwa viongozi na wananchi wanaosimamia miradi ya Halmashauri ya Wilaya, wasimamie na wafuatilie miradi kwa ubora na miradi ikamilike kabla ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuisha.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo, wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanyika Qamtananat, Maretadu juu, Maretadu, Masakta, Dinamu, Mguruchan, Shule ya sekondari Dr. Olsen, Haydom na Endabash, April 3 na 4, 2024, Mbulu mkoani Manyara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Joseph Mandoo (wa pili kulia) akikagua miradi kata ya Maretadu akiwa na walaamu wa Halmashauri.
“Ni wajibu wetu kuhakikisha miradi hii inakamilika kabla ya terehe 30 mwezi wa tano,2024 ili majengo haya yatumike kwa makusudi yaliyolengwa, na pia yatunzwe kwa vizazi vijavyo. Kimsingi nampongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wetu wa jimbo kwa namna wanavyo endelea kuhakikisha jimbo letu na Halmashauri yetu inapata fedha nyingi. Lakini pia niwapongeze viongozi wa ngazi za vijiji na kata ambao ni wasimamizi wa miradi hiyo kwa sehemu kubwa kazi zimefanyika vizuri, ninawapongeza pia lakini wito wangu waendelee kusimamia vizuri na kuhakikisha mikataba hiyo tarehe 30 mwezi wa tano majengo yanakamilika.” Alisema Mandoo.
Madiwani, wataalamu pamoja na wananchi wa Qamtananat wakikagua mradi wa Zahanati katika kijijji hicho.
Aidha alisema malengo makuu ya ziara hiyo ya kamati ya fedha ni kuhakikisha wanakagua fedha ambazo wameletewa na serikali, wanaangalia ubora wa majengo, wanaangalia thamani ya fedha ambazo zimeletwa lakini pia na kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Kwa upande wa Afisa Mipango wa Halmashauri Haygaru Karengi amesema kuwa wananchi wanatakiwa waelewe kwamba miradi hii ni kwa ajili ya faida yao na ni kwaajili ya huduma ya jamii kwa jamii inayozunguka miradi hiyo, lakini pia wanatakiwa kujua serikali imeleta fedha nyingi kwa ajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi, kwa hiyo wanatakiwa waweze kuimiliki miradi ile, ili iweze kuleta faida na tija ambayo serikali imekusudia.
Kamati ya fedha ikikagua miradi katika kata ya Maretadu.
Naye Injinia wa Halmashauri, Joseph Muna, alisema kuwa changamoto kubwa alizoziona karibu kwenye miradi mingi ni mafundi kuwa na nguvukazi ndogo, yani kutokuwa na vibarua wa kutosha na kwa maana hiyo spidi ya kazi inakuwa ndogo, pia alibainisha kuwa kamati zinazohusika na mapokezi kutokuwa makini na mapokezi ya vifaa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.