Kutoka Kushoto ni Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Wilaya ya Mbulu, J.G.Mandoo na Katikati Mwenye Shati la Kijani ni Mhe. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,
Saimon Lulu Wakiwa Katika Ukaguzi wa Miradi ya UVIKO 19
Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Waalimu Shule ya Sekondari Bishop Hhando Kata ya Masqaroda
Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Sekondari Yaeda Ampa Kata ya Tumati
Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Waalimu Shule ya Sekondari Endoji Kata ya Tumati
Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Sekondari Alexander Saulo Kata ya Dongobesh
~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~
Haya yamejiri leo ambapo Kamati ya Siasa ya (CCM) Mkoa imekagua utekelezaji wa miradi ya Uviko 19 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo kitaifa inatakiwa kukabidhiwa tarehe 30.12.2021
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara Mhe.Saimon Lulu huku wakiwa na Kamati ya siasa ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, S.V. Makota, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wialaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli aliyekuwa na timu ya wataalama mbalimbali katika ukaguzi huo.
Kimsngi katika sekta ya elimu Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ilipokea kiasi cha Tsh 980,000,000/= kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 39 vya Shule za sekondari ikimaanisha chumba 1 Tsh. 20,000,000/= na Tsh 80,000,000/= ikiwa ni fedha za elimu kwa shule za Msingi ambazo ni shikizi kwa vyumba 4 vya madarasa. kwa kweli Utekelezaji wa vyumba vyote 43 vya madarasa ni mzuri mno na wa kiawango cha juu sana. Utekelezaji wa miradi hii kwa hatua iliyofikiwa kwa ujumla ni nzuri sana ila dosari ndogondogo ambazo hazikosekani zirekebishwa, akini zoezi la ufuatiliaji wa madawati uendelee kutoka kwa wazabuni ili wakamilishe kwa wakati katika shule chache zilizobaki.
Hata hivyo katika majumuisho kamati yote kwa ujumla wao wanashukuru kwa ushirikiano kutoka hamashauri ya wilaya ya mbulu pia wanaishukuru serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia S.H. kwa kutuletea fedha hizi kwa ajili ya kusaidia elimu katika Wilaya zote Tanzania nzima, fedha hizi ni za mkopo lakini zimegusa kila mtu hadi mwananchi wa chini kabisa na kwa nchi nzima, pia Mhe.Rais Samia S.H. yuko wazi kwa kila jambo katika hili tunamshukuru sana, kwa sasa tunaimani kwamba watoto wetu watapata sehemu nzuri ya kujisomea.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.