Ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu ikiongozwa na Komredi Malkiadi Jacob Nali imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mnamo tarehe 10/08/2023.
Komredi Nali ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dokta Samia Hassan Suluhu kwa kuleta fedha za kutosha kwa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Hakika tunayo sababu za kuendelea kujisifia na kupongeza Serikali yetu kwa kutujali wana Mbulu kwani fedha zilizoletwa na zinazoendelea kuletwa ni nyingi hii nikuonesha Serikali yetu inajali wananchi wake.
Miradi iliyotembelewa inajumla ya thamani ya Bil.1.72 ikiwa ni miradi ya Elimu, Afya,Maji na Barabara.
Wajumbe wa Kamati hiyo ya siasa baadaya kutembelea Miradi hiyo ndani ya Wilaya wamempongeza Mbunge wa jimbo la Mbulu Mhe. Flatei Massay pamoja na Madiwani wote kwa kushirikiana katika kusimamia fedha na miradi inayotelezwa ndani ya Wilaya.
Aidha tunapenda kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na timu ya Wataalam kwa kusimamia miradi vizuri na kuwataka kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kwani inapokamilika inasaidia kufikisha huduma zote kwa jamii husika,wataalam niwaombe tuendelee kuonesha utaalam wetu tuliosomea ili miradi yetu ikawe na sifa sitahiki.“Alisema Komredi Malkiadi”
Komredi Malkiadi aliendelea kusema nitafurahi kuona miradi inayoletwa inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kizuri kwani hii itaendelea kutujengea heshima ndani na nje ya Wilaya yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.