Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu Ikiwa Katika Mtambo wa Mradi wa Maji Mbulu Kulia ni Meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini Akifafanua Jambo Katika Mradi Huo.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu, Ikiwa Katika Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kata ya Dongobesh.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu, Ikiwa Katika Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kata ya Dongobesh.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu, Ikiwa Katika Mradi wa Barabara ya Lami Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kata ya Dongobesh.
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbulu Mh. Mhandisi, Melkiadi Nari Akizungumza Katika Kikao cha Majumuisho Leo Tarehe 28.09.2021.
Aliyesimama ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akizungumza Katika Kikao Hicho cha Majumuisho Leo Tarehe 28.09.2021.
~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo baada ya kamati husika kuwa na ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo kwa wananchi inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri yawilaya ya Mbulu. Kamati hii inautaratibu wa kukagua miradi ya maendeleo ili kujiridhisha kuhusiana na mapokezi ya fedha za serikali, mapato ya ndani, na utekelezaji kwa vitendo kwa hizi fedha kwenye miradi husika ili kupunguza kero za wananchi na kuleta maendeleo.
Kimsingi miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa barabara za lami makao makuu ya wilaya ya Mbulu Kata ya Dongobesh kiasi cha kilometa 10 katika mitaa ya Kata ya Dongobesh ambayo inasimamiwa na ofisi ya Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA), miradi ya maji inayosimamiwa na Wakala wa Maji Mjini na Vijijini, mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyoko Kata ya Dongobesh na mwisho ni ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1 Shule ya Sekondari Bishop Hando ambao unasimamiwa na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Katika miradi yote waliyopita kamati imeridhishwa na viwango vya hali ya juu vya ubora wa miradi na thamani ya fedha zilizotumika katika miradi yote hii kwa kila mmoja wao na kuwapongeza wataalamu kuanzia Wahandisi, Mameneja na Menejimenti kwa ujumla wao hadi kufanikisha katika hatua inayoonekana kwa sasa.
Hata hivyo Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota ambaye ndiyo mwenyeji wao kwa Wilaya ya Mbulu ameahidi kwamba ataendelea kuwasimamia wataalamu wote ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kwa wakati kiasi kwamba siku zote tuwe na miradi mizuri ya kiwango cha juu kwani miradi inapokuwa ni mizuri thamani ya fedha inaonekana hivyo wananchi kuwapunguzia kero kama mlivyoona kero ya maji imepungua, elimu kwa unjenzi wa vyumba vya madarasa na waaalimu kupata ofisi, kuwepo kwa barabara kunaongeza mvuto wa wananchi kufanya biashara na kila pahali pa mji sasa panaonekana na panapendeza.
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu anaishukuru sana serikali kwa kuleta fedha hizi katika Wilaya ya Mbulu anaomba kuendelea kuongeza katika miradi mingine kwa hawa wananchi kwani fedha zote zitatumika kwa kufuata kanuni na taratibu za kisheria.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.