Wajumbe wa kamati ya siasa wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara ndugu Iddi Mkowa, wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya bilioni 41. Aidha ndugu wajumbe wamewapongeza wananchi kwa kuamua kukilinda chanzo cha maji ambacho leo hii kimekuwa chanzo adhimu kwa upatikanaji wa maji kwa wilaya ya Mbulu.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza, katibu wa CCM Mkoa amewaambia kuwa Rais Samia anawapenda sana na ndio maana miradi mingi ya kimkakati imeelekezwa kwao.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi Mhandisi Onesmo Mwakasege amesema mradi huu unatekelezwa katika vijiji 21 vilivyoko halmshauri ya Wilaya ya Mbulu,aidha mradi huu unatekelezwa kwa vyanzo vitatu vya fedha ambazo ni fedha za Serikali kuu, P4R na Fedha za mfuko wa Maji ambapo mradi utakamilika kwakipindichasiku 730.
Mhandisi ameiomba kamati ya siasa kuweza kufanikisha upatikanaji wa fedha za mradi kwa wakati ili iweze kukamilisha mradi huo kwani Mkandarasi anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa kukosa fedha kwa muda saa.
Akiongea kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bi.Queen Sendiga amehaidi kutuma wataalam wake Wizara ya Maji ilikuhakikisha wanafuatilia fedha hizo ili kumpa nafasi mkandarasi kukamilisha mradi nakuwezesha wanufaika wa mradi wanapata Maji Safi na salama.
Nae katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Manyara Comrade John Nzwalile akiwasalimia wananchi amewaambia kuwa CCM iko kwa ajili yakutekeleza ilani yake nakuhakikisha wananchi wote wa vijiji 21 wanafikiwa na Maji
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.