Na, Ruth Kyelula, Mbulu – DC.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima amesema kuwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara hakiwezi kukaa kimya kwa kipindi cha miaka mitano badala yake kimefanya ziara ya ukakguzi wa miradi ili kuona Ilani ya uchaguzi inayootekelezwa kwa vitendo, ili waweze kugusa ustawi, maendeleo na mabadilliko ya maisha kuwa bora kwa wananchi wanaowaongoza.
Hayo yalisemwa May 28,2024, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, wakati kamati ya siasa mkoa ikihitimisha ziara yao ya siku sita ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mkoa wa Manyara.
Kamati ya siasa Mkoa wa Manyara walipotembelea Daraja lililopo Garkawe kata ya Maretadu
“Huu ni utaratibu wa chama, na ndio maana kwa siku sita tumekuwa katika hii kazi, tunatoka tunaenda saiti na sio kwamba serikali hatuiamini lakini ni muhimu na sisi tukajionea, kuona ni kuamini, tukaone ilani yetu inayotekelezwa kwa vitendo, Mkuu wa Mkoa naomba nikuhakikishie kwamba, umetupitisha katika Wilaya zako zote kuanzia Kiteto na leo tunaishia hapa Mbulu, kwa sababu ratiba imetimia na tunahitimisha vizuri kabisa, na tunahitimisha hapa Mbulu, sisi wenyewe tumeridhika.” Alisema Mwenyekiti CCM Mkoa, Peter Toima.
Aidha Toima alisema kuwa, wananchi wa Mbulu wanafanya kazi kwa bidii sana,ukienda maeneo mengine huwezi ona hiki kitu lakini ukija Mbulu unaona, mfano ni Maretadu, wananchi wameleta mchanga na mawe wenye thamani ya shilingi milioni kumi, kwahiyo hiki kitu cha mchango wa wananchi tusikipuuze na kiweze kujitokeza kila wakati katika miradi inayotekelezwa.
Daraja lililopo Garkawe kata ya Maretadu
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga alimuahidi Mwenyekiti wa chama Mkoa kuwa wao kama serikali wataendelea kutekeleza maelekezo ya chama, kwa maana ya kuhakikisha wanatoa miradi mizuri yenye ubora na kunamaliza katika muda unaotakiwa, lakini kikubwa Zaidi thamani ya fedha iliyotoka inakwenda kuonekana katika miradi iliyotekelezeka. Na miradi itakayokuwa na changamoto tutakimbizana nayo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbulu, Comredi Melkiadi Naari aliwashukuru kamati ya siasa Mkoa kwa kuja kutembelea katika Wilaya ya Mbulu, mana ujio wao ni chachu ya kuamsha maendeleo na maelewano ndani ya Mbulu yetu.Na tumeona chama kimewafanyia mema mengi wana wa Mbulu.
Pia alisisitiza utamaduni wa wananchi na umuhimu wake katika kujitolea katika shughuli za maendeleo hasa vijana. Lakini tunashukuru Mkuu wetu wa Wilaya anaendelea kuamsha utamaduni huu uendelee.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.