Na, Ruth Kyelula, Mbulu – DC.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbulu, Komredi Melkiadi Naari, ameongoza kamati ya siasa ya Wilaya na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya Bilioni 1,547,950,000/=.
Kamati ya siasa Wilaya wakiwa kwenye ukaguzi wa daraja Garkawe Maretadu.
Ziara hiyo ilifanyika May 25, 2024, na kupita katika mradi wa Daraja la Garkawe lenye thamani ya sh.470,950,000/= na kukagua ujenzi wa wodi tatu na vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya yenye thamani ya Bilioni 1,100,000,000/=.
Mwenyekiti Comredi Naari alimpongeza Mhandisi Nuru Hondo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa daraja la Garkawe, na kuahidi watamtunuku cheti cha mfanyakazi bora.
“Najua umefanya kazi na Mkurugenzi mtendaji, Mkurugenzi nawe tunakushukuru kwa niaba ya watendaji wenzako wa halmashauri, madiwani na ofisi yetu ya DC nayo tunaishukuru, mana bila ninyi bwana Nuru asingeweza kuvuka.” Alisema Comredi Naari.
Aidha Comredi Naari amekazia ushirikiano baina ya vyombo vitatu, Wananchi, Halmashauri, Chama na Serikali yake, na kuomba ushirikiano uwepo. Pia alisisitiza ushirikishwaji wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo na wao kushiriki kutoa nguvu kazi zao kwenye miradi hiyo ili kupunguza matumizi ya fedha ambayo ingeweza kusaidia kazi zingine.
Kamati ya siasa Wilaya ya Mbulu wakiwa kwenye ukaguzi katika hospitali ya Wilaya
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Veronica Kessy, amesema kuwa wahandisi wafuate maelekezo na miongozo ambayo inaletwa toka wizara na TAMISEMI, na kujifunza kuitekeleza. Lakini pia aliwaambia wasiache kushauri na kushirikisha menejimenti pale wanapoona fedha haziendani na uhalisia wa mradi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Veronica Kessy akisisitiza jambo katika ziara ya kamati ya siasa Wilaya katika hospitali ya Wilaya.
“Mkurugenzi andaa nyaraka zote, miongozo, BOQ pamoja na ramani ya miradi yote kuanzia hapo hospitali, kituo cha afya, yote ikae tayari.” Alisema mkuu wa Wilaya Veronica Kessy.
Naye Katibu wa Chama cha CCM Wilaya ya Mbulu, Grace Haule aliwaomba CMT kwa umoja wao wamsaidie Mkurugenzi katika kutekeleza mambo mbali mbali ya halmashauri ikiwemo miradi ya maendeleo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.