Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Katika Uhamasishaji Kata ya Maretadu na Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Bi. Sara Sanga.
Kaimu Mganga Mkuu Dr. Shirima Katika Uhamasishaji Kata ya Maretadu.
Nyenzo za Uhamasishaji Zinawekwa Sawa Kwa Kuongeza Mafuta Kwenye Jenereta, Kata ya Eshkesh.
Bw. Edes Malley wa Kitengo cha Matangazo Katika Kamati Hii ya Wilaya ya Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Eshkesh.
Zoezi la Uchanjaji Likiendelea Baada ya Uhamasishaji wa UVIKO 19 kueleweka, Kata ya Eshkesh.
Baada ya Kazi Hapa ni Masuala ya Chakula Huko Huko Porini, Kata ya Eshkesh.
Kamati ya Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Endamilay.
Zoezi la Uhamasishaji UVIKO 19 Likiendelea, Kata ya Endamilay.
Wananchi Wakiuliza Maswali Katika Mkutano Huo wa Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Endamilay.
Kamati ya Wilaya ya Uhamasishaji UVIKO 19, Wakiwa Kata ya Endamilay.Padri Kanisa la Roma Gidhim.
Zoezi la Uhamasishaji Likiendelea Ndani ya Kanisa la Roma Baada ya Kupata Idhini ya Padri.
Waumini wa Kanisa Hilo.
Zoezi la Uchanjaji Lilinaendelea Baada ya Uhamasishaji wa UVIKO 19 Kueleweka, Kanisa la Gidhimi na Roma Dongobesh.
Zoezi la Uhamasishaji wa UVIKO 19 Likiendelea Katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Eshkesh.
~~~~~~~~~~ HABARI KWA UNDANI ZAIDI ~~~~~~~~~~
Mafanikio haya yamepatikana kwa ushirikiano wa dhati toka kwa Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota ambaye alifungua kampeni hii tarehe 30.09.2021 Kata ya Maretadu ambapo takribani watu wapatao 50 walichanjwa katika kampeni hiyo pale pale na kuendelea katika maeneo mengine kwa wilaya nzima kwa msisimko ule ule.
Hadi tarehe 13/10/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechanja jumla ya watu 1447 kati ya dozi 1675 na kubaki 25 tu. Awali kama Wilaya ilipokea chanjo aina ya "Jansen n Jansen" ya Marekani dozi 2000 lakini dozi 325 zilichukuliwa na Hospitali ya Mkoa kwenda kutumika huko baada ya mahitaji kuwa mengi zaidi ya dozi walizonazo na hili ni jambo la kawaida kwa utendaji kazi wa afya kote nchini, lakini dozi 205 ziliharibika kutokana na sababu mbalimbali.
Katika hali ya kuhakikisha wananchi wote wanaendelea kufanya kazi zao vizuri kiuchumi, kijamii, ndani na nje ya nchi hatimaye kuwa salama na gonjwa hatari la UVIKO 19 Mh. Mkuu wa Wilaya alihamasisha kwa nguvu zote, kijiji kwa kijiji kata hadi kata ili tu elimu iwafikie itakayopelekea wananchi kuwa na mwamko wa kuchanja UVIKO 19 bila shida. Kisha timu ya Wilaya ya UVIKO 19 iliyopata mafunzo kimkoa iliendelea na kampeni ya uhamasishaji kwa kasi katika maeneo yenye watu wengi, kwenye matukio na popote ambapo pana shuguli za kiuchumi na kijamii kuanzia viwanja vya mpira, stendi za mabasi, sokoni, mitaa ya biashara na vijiji hadi kwa wavuvi Yaeda chini na Eshkesh.
Imefahamika kutoka kwa Wataalamu wa afya kwamba hakuna madhala wakati na baada ya kuchanja kama inavyosemekana na wengi kwani cha kwanza kabisa hutaweza kuambukizwa tena na UVIKO 19 na ikitokea ukapata basi hutaathirika kwani kinga zitakuwa zimeimarika sana kutokana na mwili kujijengea kinga ya awali iliyotengenezwa kutokana na chanjo iliyoko mwilini, wakati huo huo ambaye hajachanjwa akiambukizwa anakuwa hana kinga ya kutosha lakini mbaya zaidi hutumia gharama kubwa sana katika kujitibu ambapo kwa utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya nchini Tanzania imejulikana kwamba ni kati ya Tsh. 200,000 hadi Tsh. 300,000 kwa siku gharama za kuokoa uhai wa mgonjwa wa UVIKO 19 kwa kununua mitungi ya kuongeza heya ya "Oxygen" tu, hivyo wananchi wanatakiwa kufanya juu chini kuchanja, kwasababu ndiyo kinga pekee hadi sasa kwani hakuna dawa ila watabibu wote hutibu dalili inayojitokeza kwa mgojwa; mfano kama anaharisha atatibiwa kuhara ili asiendelee kuharisha.
Maswali yanayoulizwa mengi ni kwamba binadamu baada ya kuchanjwa atapata ugumba jambo ambalo sio kweli wanaume kwa wanawake wanaendelea na uzazi wao kama kawaida, juu ya suala wajawazito na wanaonyonyesha imefahamika kwamba hayo ndiyo makundi yaliyo hatarishi zaidi kwani kinga zao zinakuwa zipo chini kutokana na hali aliyonayo hivyo yeye anapaswa achanje na haina madhara kwa mama na mtoto aliyepo tumboni au anayenyonya pia.Kuna wanaouliza kwamba hubadilisha vinasaba vya binadamu yaani "DNA" hiyo si kweli kwani chanjo yoyote ili ibadilishe Vinasaba "DNA" basi ni lazima iingie kwene kiini cha seli husika ambayo kitaalamu inaitwa "Neuclear" ambapo chanjo hizi haziingii kwene kiini cha seli bali hufanya kazi sehemu ya nje tu na haina kiwezeshi chochote cha protini cha kuifanya iingie ndani ya kiini "Neuclear" na kukaa humo.
Pia wapo wanaouliza kwa nini imefanyika kwa haraka haraka hivi ukilinganisha na chanjo zingine zinachukua hadi miaka 10 ndipo ianze kutumika kwa mwanadamu? katika kujibu hili ni kwamba huu ugonjwa wa mafua unaotokana na kirusi haujaanza leo kwasababu kwa takwimu zilizopo duniani ulikuwepo mwaka 2002 ugonjwa wa mafua ujulikanao kama "SARS" na kisha ukafuata "MARS" huko uarabuni uliua sana watu, yakaja mafua ya ndege, na baadaye mafua ya nguruwe na mengine mengi ambapo mwanadamu katika kukabiliana na hili alishaanza utafiti kupitia Shirika la Afya Duniani "WHO" na taasisi zingine mbalimbali za kimataifa lakini kwakuwa magonjwa haya yalikuja kutoweka yenyewe basi ikawa tafiti zote za kisayansi kutoendelea na kukoma baada ya dunia kuwa salama.
Hivyo baada ya huu ugonjwa wa UVIKO 19 kuonekana tena watafiti wale wale wakaanzia pale pale walipoishia na utafiti wa awali kiasi cha kupelekea kupata majibu mapema. Jingine ni kwamba kwa sasa utaalamu wa kibinadamu katika kuchambua mambo umeongezeka tofauti na miongo 3 iliyopita, vifaa na teknolojia ya kitabibu navyo vimeongezeka kwa kiwango cha ajabu kabisa jamba ambalo ukokotoaji wa data za sampuli za kitu chochote hutumia muda mfupi kutokana na vifaa tehama vya sasa kuwa vya kisasa zaidi na vya kimamboleo kwa maana ya uwezo wa hali ya juu sana. Mfano hai ni hesabu iliyokuwa inafanywa siku 3 kwa kompyuta ya miaka ya 1950 kwa sasa inatumia sekunde tu kufanya kitu kile kile, sababu nyingine ni kwamba ugonjwa wa UVIKO 19 unasambaa kwa haraka kwa watu wengi na pia humuua mgojwa kwa haraka sana ambapo kitabibu imesaidia kumfuatilia mdudu husika yaani kirusi namna anavyoathili mwili na hivyo kupata majibu ya mapema ya mzunguko wa majaribio ya dawa husika kwa haraka ukilinganisha na magonjwa mengine ya chanjo yanayochukua muda mrefu hadi mtu kuathirika vibaya.
Kwa nini tuiteue "Jansen n Jansen" ya Marekani, ni kwamba ndiyo chanjo inayoweza kuhifadhika kwa mazingira yetu hadi vijijini kulingana na vifaa tulivyonavyo yaani nyuzi joto la 2C hadi 8C tofauti na zingine zenye hadi nyuzi joto hasi -50C, lakini pia ndiyo chanjo ya kwanza kuifanyia uchunguzi kwa madaktari bingwa wa Tanzania katika kituo cha utafiti kilichopo Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine "SUA"
Kama ni kupata homa au maumivu kiasi kwa siku 2 au 3 za mwanzo ni kwa baadhi ya watu lakini ndiyo kawaida ya dawa yoyote ambayo huwa ngeni mwilini mwako kama ilivyo chanjo zingine pamoja na madawa mengine ya magonjwa ya maralia, "typhoid" na mengine mengi kwamba ukisha kunywa tu basi mwili katika kupokea dawa hizi utajiskia hali fulani lakini haimaanishi haitakutibu malalia au "typhoid" uliyonayo, mbona klorokwini za homa kwa kipindi fulani hivi watu walikuwa wanawasha sana na pia "Metachelfine" inakunyong'onyesha kabisa na mwili kulegea lakini huwa ndio kupona kwenyewe.
Hata hiyo kama Rais wetu Mhe. Samia S. Hassan amechanjwa na Mawazili, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, wataalamu wa afya, Mameneja na Wakuu wa taasisi zote za serikali wamechanjwa hii inaonyesha namna gani inavyoaminika kuwa ni salama na kwako pia.
Vituo vya kuchanjia ni sehemu zote za kutolea huduma ya afya kuanzia Zahanati, Vituo vya afya na Zospitali zote za Wilaya huku gali la kliniki linayotembea hutoa pia huduma hiyo popote linapokuwa linatembea ili kumrahisishia mwananchi kupata huduma kwa haraka vijijini, lakini hata kama wewe ni mwananchi na mkazi wa Mbulu wilaya uko Dar es salaam, Mwanza au mbeya au popote unaruhusiwa kwenda kituo chochote cha kutolea huduma ya afya kilicho karibu nawe utapa chanjo hii na usaidizi wa maelekezo mengine ya Daktari.Serikali itaendelea kupokea aina zingine za chanjo zitakazothibitishwa na madaktari wetu bingwa wa hapa nchini kama vile chanjo ya "Sinopharm" ya China na sisi hatuwezi kukaa kama kisiwa kwani nchi zote zinautaratibu huu duniani wa kuchanja chanjo hii hii.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.