Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James mapema leo amefanya ziara katika kata ya Eshkesh na Yaeda Chini zilizopo katika jimbo la Mbulu vijijini, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kwa kata zote yenye lengo la kukagua miradi, kuhamasisha shughuli za maendeleo, na kusikiliza kero za Wananchi.
Akiwa katika kata hizo mbili, Komred Kheri James amewahimiza Wananchi kuzingatia mpango wa matumizi bora ya Aridhi ili kujiwekea uhakika wa maeneo ya malisho ya mifugo, maeneo ya kilimo na kuendelea kunufaika na fedha zinazo tokana na biashara ya hewa ya ukaa inayo fanyika katika Kata hizo kwa ushirikiano na Taasisi ya Carbon Tanzania.
Aidha Komred Kheri James amewaeleza wananchi kuwa mpango wa matumizi bora ya aridhi utasaidia kupunguza migogoro ya aridhi na utasaidia kupunguza changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi yanayo tokana na Uharibifu wa mazingira unaofanywa na Shughuli za binaadamu.
Katika ziara ya leo Mkuu wa wilaya ametembelea miradi ya elimu yenye thamani ya shilingi milioni mia tano, na amepokea mipango ya maendeleo iliopangwa na kila Kata kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo pamoja na kusogeza na kuimarisha huduma kwa wananchi.
Ziara hiyo imehudhuriwa pia na Kamati ya Usalama, Viongozi na watumishi wa Halimashauri ya wilaya ya Mbulu, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wananchi.
#KwaPamoja,Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.