Na, Ruth Kyelula, Afisa Habari Mbulu DC.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Muhaji amewataka watendaji na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kuzingatia vipaumbele vyake vinne katika utendaji kazi wa shughuli za kila siku za Serikali
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala mkoa wakati wa kikao kifupi na watendaji na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Februari 01, 2024.
“Jambo la kwanza ni ukusanyaji wa mapato, la pili mkasimamie vizuri miradi ya serikali na mpambane kuondoa miradi viporo ili miradi iweze kukamilika kwa wakati,la tatu mkajitahidi kutoa huduma bora kwa wananchi, mkatatue kero za wananchi na la nne mkazingatie matumizi bora ya fedha za serikali.” Alisema bi. Maryam.
Katibu Tawala akiongea na wakuu wa Idara wa Mbulu DC
Mbali na hayo Katibu Tawala aliwaasa watumishi wa Mbulu DC kuwa na mahusiano mazuri ya utendaji kazi baina ya mtumishi na mtumishi na kuacha chuki binafsi badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kuweza kutatua kero za wananchi.
Katibu Tawala wa Mkoa bi.Maryam Muhaji wa nne kushoto, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mbulu DC, Abubakar Kuuli , wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa idara wa Mbulu Dc.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Abubakar Kuuli, alimshukuru Katibu tawala kwa kutenga muda wake na kuja kujitambulisha kwa wafanyakazi wa Halmashauri na kumuahidi kutekeleza yale yote maelekezo aliyoyatoa katika ziara yake hiyo na aliahidi kumpa uushirikiano katika kipindi chake chote cha uongozi
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.