Ng’orat ni miongoni wa vijiji 76 vilivyopo halmashauri ya wilaya ya mbulu, katika kudhibiti magonjwa ya mifugo wananchi wa Kijiji Cha Ng'orati kilichopo kata ya Ghidihim kimeweza kuogesha ng'ombe 822,mbuzi na kondoo 483. Zoezi hilo lilifanyika siku ya ufunguzi wa josho la kuogeshea ng'ombe mnamo tarehe 14 Julai 2023.
Mkuu wa kitengo Cha Mifugo na uvuvi Mr. Moses Nduligu ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji Cha Ng'orati kuwa, wanatakiwa walilinde josho hilo lililozonduliwa na walione kama mali yao kwani ni muda mrefu kijiji hicho kimekaa bila josho.
"Wanakijiji muone hilo josho ni mali yenu, kwa sababu mmeshiriki kwenye ujenzi kwa kuweka Nguvu zenu za kuleta mchanga, mawe,kokoto, maji na kuchimba shimo.Ambapo mchango wa wenu ni milioni sita kitu ambacho tunajivunia nanyi”. Alisema Nduligu
Mr. Moses aliendelea kusema kuwa wanakijiji wote wenye mifugo wahakikishe wanaogesha mifugo yao kwa sababu lengo lilikua kupunguza magonjwa ama kuondoka kabisa magonjwa yanayosababishwa na kupe, magonjwa ambayo ni hatari sana kwa ng'ombe na wafugaji.
kwa sasa majosho ambayo yameshakamilika kwa hatua za ujenzi ni la Ng'orati, Bashay, Yaeda chini na Masoderere. Ambapo Kila ujenzi wa josho moja unagharimu zaidi ya shilingi milioni kumi na saba.
Kwa upande wake Afisa mifugo Apolinary Bura, alisema kuwa changamoto ya Josho ilikuwepo muda mrefu, ambapo ng'ombe hawakuwa wakiogeshwa ambapo ikipeleka ng'ombe kuugua na kudhoofika. Aidha umbali wa majosho ulipelekea ng'ombe wengi kupotea wanapochanganyika na wengine.
kutokana na changamoto hizo idara ya Mifugo walipata wazo la kuongeza majosho kwa kila kijijij, na miongoni wa vijiji hivyo ni kijiji cha Ng’orat ambapo wanakijiji walilipokea wazo hilo na mwamko wao wa kushiriki ulikua mkubwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ng'orati Stephen Ammo amewaomba wanakijiji kutunza miundombinu ili iendelee kuwanufaisha kwa muda mrefu. Lakini pia ameiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kwa sababu uelewa wa wananchi kuhusu magonjwa ya kupe ni mdogo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.