Kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi katika Mji wa Dongobesh halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kujadili na kupitisha kwa kauli moja mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika halmashauri hiyo ikiwa baraza hilo limebakisha kuketi kwa mara ya mwisho hapo baadae mwaka huu kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2020
Katibu wa Baraza la Madiwa(Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndugu. Kamoga) akifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa ziwasilishwa mezani.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mbulu Hadson Kamoga, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, wakuu wa Idara mbalimbali katika Halamshauri hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Ndugu Simbalimile Mufoga akitoa salama za Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay akichangia mambo mbalimbali ndani ya jimbo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh. amewataka wataalamu wa kilimo kwa kushirikiana na madiwani wa kata zote katika eneo hilo kufanya tathimini ya uharibifu wa mazao ili kuweza kuwa na takwimu sahihi ya hali ya chakula kwa mwaka huu
Akiongezea kuwa kwa kutokuwa na takwimu sahihi itakuwa ni vigumu sana kutambua changamoto zitakazojitokeza hapo baadae na hii ni kutokana na tishio lililopo la wadudu aina ya Nzige ambao tayari wapo nchi jirani ya Kenya ambao tayari wameshaingia nchini Uganda kwa hapa nchini wamekwishaanza kuingia katika Mkoa wa Kilimanjaro
Baadhi wa Waheshimwa Madiwa walipokuwa katika Ukumbi wa Mkutano kuendelea na Baraza.
Aidha kwa upande wa madiwani wamewasilisha taarifa za usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata zaote ikiwa ni mara ya kwanza kwa baraza hilo kuwasilisha ripoti hizo huku wakipata nafasi za kuhoji, kuchangia mambo mbalimbali katika ripoti hizo pamoja na kutoa maoni
Kutoka kushoto ni Wakili Msoni Mhe. Green pamoja na Katibu wa Vikao ndugu Mulokozi wakiteta jambo wakati wa kikao cha Baraza.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Badhi ya Wataalamu wa Hlamashauri wakiwa ukumbini
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.