Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ni miongoni wa halmashauri zinazotekeleza agizo la Mhe.Rais kwa kutoa mikopo ya asilimia 40 kwa Wanawake, asilimia 40 kwa Vijana na asilimia 20 kwa Walemavu.
Komredi Heri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu akikabidhi pikipiki kwa Kikundi cha Tupendane cha Labay.
Akikabidhi mkopo wa pikipiki tano kwa kikundi cha Tupendane cha vijana toka kata ya labay, komredi Heri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ameipongeza halmashauri kwa kuendeleakuteleza ilani ya chama ipasavyo kwa asilimia mia na amewaomba vijana waliopata mkopo huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili waweze kurejesha mkopo kwa wakati na mwisho wa siku waweze kujiendesha bila kuwa na mkopo.
Viongozi mbalimbali wakiongozwana kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya nabaraza la Madiwani wakifurahi kwa pamoja mara baada ya kukabidhi Mkopo wa pikipiki kwa kikundicha tupendane.
Akiongea kwa niaba ya baraza la Madiwani la halmshauri hiyo,Mhe Joseph G. Mandoo amesema wananchi wanaochukua mikopo kuhakikisha kuwa wanakuwa mifano katika jamii kwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufaidiki na kile wanachokikopa,na pia ametoa wito wananchi wajitokeze kuomba mikopo.
Tumeshatoa mikopo kwa awamu mbalimbalina kwa vikundi mbalimbali ndani ya halmshauri ya Wilaya, na mikopo hii ikiwa ni awamu ya pili tumeweza kuvikopesha vikundi mbalimbali kama vile One Vision toka Dongobesh, Sangamyanda cha Gidhim, Tupendane cha labay na vinginevyo vingi, ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji ndugu Abubakari Kuuli
wanakikundi wakiwa tayari kuondoka mara baada ya kukabidhiwa pikipiki zao
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.