Na Ruth Kyelula, Mbulu DC
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Moses Nduligu, amesema kuwa wamewapa Kitengo Cha Lishe bajeti ya kuanzia ya shilingi milioni 56 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za mambo ya Lishe kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo itaweza kuongezeka muda wowote kadiri ya mahitaji .
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili bajeti ya Lishe ya mwaka 2024/25 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri, ulipo Dongobesh, December 02,2023.
Aidha kaimu Mkurugenzi amewataka Wakuu wa Vitengo na Idara waweke bajeti ya mambo ya Lishe, kwa sababu Lishe ni kitu cha muhimu na cha lazima kwenye Halmashauri, lazima ionekane kwa Kila Idara imeweka bajeti hiyo.Lakini pia jamii ihamasishwe kuhusu kutumia Lishe kwa mfano ma shuleni, lakini pia iwe ajenda mtambuka iende kwenye vikao vyote vya Taasisi hata vikao vya jamii.
Kwa upande wa Afisa Lishe wa Wilaya Jackline David amesema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imewapatia Kitengo Cha Lishe kiasi Cha milioni 56 kwa ajili ya kutekeleza afua mbalimbali za mambo ya Lishe.
Afisa Lishe alisema kuwa kiwango hicho huwa kinatengwa kulingana na idadi ya watoto chini ya miaka mitano ambao wapo kwenye Halmashauri yetu. Alisema kuwa kwa taifa huwa Kuna kiwango kwamba idadi ya watoto ulionao, Kila mtoto anatakiwa atengewe angalau shilingi Elfu moja.
"Halmashauri yetu imekidhi viwango vya kumpa Kila mtoto shilingi elfu moja na mia mbili, kwa sababu sisi tuna jumla ya watoto 50388, kwahiyo Halmashauri yetu imevuka lengo la Kitaifa, la shilingi elfu moja kwa Kila mtoto tuweweza kumpa elfu moja mia mbili Kila mtoto. Kwahiyo kwa mwaka ujao wa fedha Halmashauri imetenga milioni 56 kwa ajili ya kutekeleza afua za Lishe." Alisema Afisa Lishe.
Afisa Lishe alisistiza wananchi wa Wilaya ya Mbulu wazingatie elimu wanazowapa, maelekezo wanayowapa mfano kwa wazazi wanawaelekeza namna gani ya kuandaa chakula kwa watoto na wawalishe kwa muda gani, lakini pia wanawahimiza wamama wajawazito kuwahi clinic ili waweze kupata huduma za awali ambazo mama mwenye matatizo ya kiafya kuweza kumkinga mama na mtoto, maambukizi yale ya mama na mtoto lakini pia atapatiwa vidonge vya virutubishi vya nyongeza ikiwemo vidonge vya madini chuma ambavyo pia vitamkinga mtoto na matatizo mengine ambayo ni pamoja na mgongo wazi, midomo sungura, mtoto kuzaliwa na ulemavu. Zile wiki kumi na mbili za mwanzo ni muhimu kwa sababu ndio kipindi viungo vya mtoto hutengenezeka.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.