Aliyesimama ni Mgeni Rasmi Ndg. Abubakar A. Kuuli Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kny: Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Akitoa Nasaha Kwa Wahitimu Hao Katika Mahafali Hayo Yaliyofanyika Viwanja Vya Taasisi Hiyo Haydom Tarehe 22.07.2022
Mgeni Rasmi Ndg. Abubakar A. Kuuli Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Akielea Kwenye Ukaguzi wa Majengo Mbalimbali na Kuona Huduma Zinazotolewa na Taasisi Hiyo.
Mgeni Rasmi Ndg. Abubakar A. Kuuli Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Akipewa Maelekezo Mbalimbali Katika Ukaguzi Huo.
Mgeni Rasmi Ndg. Abubakar A. Kuuli Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Kny: Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Akiweka Jiwe la Msingi Katika Jengo la Utawala KatikaTaasisi Hiyo.
Shangwe, Nderemo, Hoihoi na Vifijo Vilitawala Katika Mahafali Hayo Kama Unavyojionea Mpenzi Msomaji.Maandamano Yakiongozwa na Mgeni Rasmi Kuelekea Viwanja Vya Taasisi Hiyo kwa Sherehe.Mgeni Rasmi Ndg. Abubakar A. Kuuli Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Kny: Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Katika Nasaha Kwa Wahitimu.
Zoezi la Mgeni Rasmi Kunuku Vyeti kwa Wahitimu
Picha Mbalimbali
~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo tarehe 22.07.2022 katika mahafali ya 5 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi ya Afya Haydom yaliyofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo ndani ya eneo la Hosptali ya Kilutheri ya Haydom. Awali mahafari hayo yalikuwa na mambo mbalimbali ya uzinduzi wa jengo la Maabara ya utengenezaji dawa (Pharmacy Laboratory Building) uliogharimu TShs. Milioni 41.1 lililozinduliwa na Baba Askofu Nicolous Nsanganzelu wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheli Dayosisi ya Mbulu, iliyofuatiwa na uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la utawala (Administration Building) na ndugu Abubakar A. Kuuli Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Charles M.Nyerere ambapo jengo hili kwa mujibu wa Mhandisi Noel J. Mphuru ni la ghorofa 5 lakini litajengwa kwa awamu ambapo awamu hii ya kwanza imegharimu kiasi cha Tshs. milioni mia 700.6 na ujenzi haujasimama unaendelea.
Katika kuhakikisha jengo hili linakamilika kwa wakati ili kuwezesha wananchi kupata huduma ya afya bora mgeni rasmi huyo alieendesha harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa jengo hilo la utawala ambapo kiasi cha Tshs. milioni 17.5 zilipatikana kwa mchanganuo wa Tsh. milioni 5.8 ilipatikana taslimu na ahadi za wadau mbalimbali ni Tsh. milioni 11.1 pia wakiwemo wahisani wa nje yaani "Norwegian Donners" ambao wao wametoa kiasi cha Norwegian Krone (NOK) 400,000/= ambayo ni sawa na kiasi cha Tsh. 600,000/=.
Mgeni rasmi katika kuwaweka sawa wahitimu ambao tayari wako na ari ya kupata ajira serikalini ametamka kwamba ni kweli serikali itaendelea kuajiri wataalamu hawa lakini pale inaposhindikana kuajiriwa serikalini siyo mwisho wa maisha bali zipo njia mbadala za kujikwamua, ikiwemo ya kujiunga katika vikundi vya wataalamu wasiopungua 5 na kupata mikopo kedekede kupitia mfuko wa wanawake, vijana na walemavu katika Halmashauri zote nchini kisha kupata mtaji na kujiajiri katika nyanja mbalimbali zenye tija kwa malengo mtakayojiwekea ya uzalishaji au utoaji wa huduma.
Mgeni rasmi huyo akaenda mbali zaidi kwamba katika kutafuta fedha za kuwa tajiri si lazima utegemee tu taaluma uliyosomea ndiyo ikutoe tu, bali unaweza angalia je wewe mwenyewe una kipaji gani ambacho wenzio hawana fanya hicho kama vile "Recreation and Entertainment" kwani ni sanaa pana ambayo inaajiri watu wengi na kunufaika kwa muda mfupi sana kuanzia muziki, maigizo, vichekesho, ufugaji, kilimo na vingine vingi usidharau kazi angalia inakuingizia kiasi gani kwa mwaka, tumieni mitandao kupata taarifa za kujiendeleza kiuchumi na kuongeza kipato badala ya kukaa kuwalalamikia wazazi na serikali lakini wengine wapo mtaani wanapiga kazi na wanamaisha sawa na watumishi na wengine mitaji mikubwa zaidi ya watumishi serikalini hivyo mlango upo wazi ni wewe kuwa na maono ya kutaka kujikwamua.
Masuala mengine mgeni rasmi aliyosisitiza katika halaiki hiyo ni kuwa na lishe bora kwa kila mtu na kwa upekee kwa akina mama wajawazito kuwa na lishe bora ili kupata watoto wasio na matatizo ya ubongo. Kwa sasa mazao mengi yanatoka kwa kuuzwa lakini tukumbuke kuweka akiba kwa ajili ya matumizi ya familia pia ukatili wa kijinsia nao upo miongoni mwa jamii zetu hivyo mjitokeze wanaume kwa wanawake pamoja na vijana ambao mnafanyiwa ukatili huu ili muweze kusaidiwa.
Katika miezi ya karibuni kulifanyika zoezi la kitaifa la anwani za makazi ambapo ni muhimu kama mtu nyumba yake haina anwani za makazi awaone viongozi wa eneo husika ili aweze kusaidiwa ina umuhimu mkubwa sana kwa maslahi ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla kwa huko mbele katika kupata huduma za afya, zimamoto, biashara na vingine vingi. Tarehe 23.08.2022 watanzania wote tunaenda kuhesabiwa maarufu kama sensa ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10 kwa nchi nyingi duniani kwa lengo la kujua takwimu mbalimbali ikiwemo idadi ya watu katika nchi husika, ili kusaidia taifa kupanga mipango ya maendeleo katika sekta mbalimbali kwa hiyo ni muhimu sana mtoe ushirikiano kwa wataalamu watakaohusika kwenu.
Furaha, shangwe, nderemo, hoihoi na vifijo vilitawala uwanja mzima kwa wazazi, marafiki ndugu na jamaa pamoja na wahitimu katika zoezi la mgeni rasmi kutunuku vyeti, ambapo kitakwimu ni jumla ya wahitimu 116 kati ya hao wahitimu wa kada ya Utabibu (Clinical Medicine) 80 na wahitimu wa kada ya Mafunzo ya Maabara (Clinical Laboratory) 36, mgeni rasmi aliwatakia heri na baraka pindi watakapoanza maisha mapya ya uraiani.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.