Aliyesimama ni Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Guulo Mandoo Akifungua Kikao cha Robo ya 4 cha Baraza la Madiwani Kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 Tarehe 27.08.2021
Kutoka Kushoto ni Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Guulo Mandoo wa katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar Abdullah Kuuli, wa Mwisho ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. S.Sanga. Aliyesimama ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mh. Flatei Akizungumza Katika Kikao Hicho
Aliyesimama ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. S.Sanga Akizungumza Katika Kikao Hicho
Secretarieti ya Vikao Kutoka Kulia ni Bw. Mlokozi na wa Pili Yake ni Bw. E.Samata.
Wafuatao Hapo Chini ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Waheshimiwa Madiwani Wakiwasilisha Taarifa Husika Picha ya Kwanza Alisoma kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Wafuatao Hapo Chini ni Waheshimiwa Madiwani Wakiuliza Maswali
Wafuatao Hapo Chini ni Wataalamu Wakiwasilisha Taarifa za Sekta Mtambuka
Wakala wa Maji Mjini na Vijijini (RUWASA)
TANESCO
Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini
Wafuatao Hapo Chini ni Wakuu wa Idara Mbalimbali Wakijibu Hoja Mbalimbali Zilizoibuliwa na Waheshimiwa Madiwani.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbulu
Wakuu wa Idara na Vitengo
Waheshimiwa Madiwani
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri leo katika baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu lililofanyika katika ukumbi wa kituo cha Elimu cha Gote Kata ya Dongobesh Mbulu. Kimsingi wakulima na wafugaji wanapata mahitaji yao mengi ya shuguli zao katika minada hii ambapo madawa ya mifugo na pembejeo za kilimo hupatikana minadani kwa bei nafuu zaidi. Imefahamika kwamba elimu inapaswa iendelee kutolewa kwani kila siku wafanya biashara wapya huongezeka ambao bado taratibu za uuzazi na utunzani wa madawa na pembejeo hizi hufahamu kwa kiasi kidogo. Kwa kuwa wataalamu wa Halmashauri walishatoa elimu hii kwa kipindi cha nyuma basi liwe zoezi endelevu kila baada ya kipindi fulani wawe wanawaelimisha wafanyabiashara hawa minadani kwa maslahi mapana ya mfanyabiashara, mkulima, mfugaji na mlaji.
Kuhusina na tarehe za minada wananchi wasiwe na wasiwasi kwani baraza la madiwa kwa kushirikiana na wataalamu wameshalipokea na wataangalia tarehe zipi ni sahihi kwa mawasiliano na maeneo husika kisha wananchi watatangaziwa upya kwasababu Halmashauri ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Vijijini.
Hata hivyo utafiti unahitajika kufanyika katika mazao mengi kama vile ngwala na dengu ili wakulima wapate mazao yanayovumilia si tu ukame bali wadudu, udongo na utoaji wa mazao mengi kwa ekari moja hii itapelekea wananchi kupata faida kubwa na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.
Pia katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuna vikundi vipatavyo 476, kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imetoa mikopo kwa vikundi 35 na kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu inakaribisha maombi mbalimbali ya fedha hizi kwa makundi yale yale ya wanawake, vijana na walemavu.
Katika sekta mtambuka yaani nishati Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mbulu amesema kwa mwaka huu wa fedha wataendelea kwa kasi zaidi kwa kufikisha umeme katika vijiji 8 huku kwa kila mwananchi ambaye ameshatoa hela Tsh.27,000/= atawekewa umeme kwani vifaa tulivyoagiza vimeshafika hivyo naimani kuanzia tarehe 01.09.2021 timu ya wataalamu wa Tanesco wataendelea na shuguli hizo kwa walioomba hata kama kuna nguzo 2 au 1 katikati tutawawekea umeme naomba mtuamini hivyo alisisitiza meneja.
Katika kikao hiki Meneja wa maji Mjini na Vijijini (RUWASA) amesema tayari miradi 4 ya maeneo ya Dongobesh, Haidared, Maghan juu na Gidimadoy vituo vyote vimekamilika na vinatoa huduma ya maji, ambapo maeneo ya Maretadu juu, Labay, Endahagchan na Gemba usanifu ulishafanyika tunasubiri fedha ili tuanze utekelezaji wa mradi. Kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 ofisi ya RUWASA inatarajia kuchimba visima 6 kwa maeneo tofauti katika Halmashauri hii.
Kwa kuongeza tija na kufanya kazi kimkakati zaidi ofisi ya RUWASA Mbulu Vijijini imepanga kununua pikipiki 9 kwa mwaka huu wa fedha ili kurahisisha usimamizi thibitifu huku shajala na vinakilishi (printa) na kompyuta(tarakilishiri) 5 zitanunuliwa ili kufanikisha kazi mbalimbali za jumuiya za maji.
Kama unavyojua vitu vyote hivi lazima vishajiishwe na uwepo wa barabara, ambapo hadi sasa kuna fedha za kuweka lami katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini yaani Kata ya Dongobesh ambapo kilometa 10 zitawekwa lami kwa mwaka wa fedha 2021/2021 kwa kufuata mahitaji na uwepo wa barabara za awali za vumbi katika Kata hii. Wakati huo huo Mji wa Haydom tutaweka kilometa 30 za Lami kwasababu mitaa ni mingi na watu ni wengi na barabara pia ni nyingi hivyo anaomba kwa wananchi kufungua njia katika maeneo yao ili kupendezesha mji kwa uwepo wa lami.
Kuhusiana na kukabiliana na UVICO 19 serikali tayari imetenga vituo 3 (Hospitali ya rufaa ya Haydom, Kituo cha Afya cha Dongobesh na Zahanati ya Muslu) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu vinavyotoa huduma ya chanjo ya UVICO 19. Serikali inatarajia kuongeza vituo vingine 4 ili kuwepo kwa vituo 7 ambapo huduma itakuwa karibu zaidi kwa wananchi.
Maandalizi ya kilimo yaendelee, lakini kwa wakulima tunasisitiza zao la alizeti ambalo ndiyo zao la kimkakati kimkoa ambapo zao hili kibiashara halimtupi mkulima kwani soko lake ni thabiti ndani ya nchi na kimataifa pia. Kwa taarifa ni kwamba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imepokea vitambulisho vipatavyo 39199 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu vijijini kwa Kata 13, hivyo tunawatangazia wananchi waende katika ofisi zao za vijiji kuchukua vitambulisho vyao; ifahamike kwamba kwa awamu ya kwanza vitambulisho hivi ni bure lakini kikishapotea ili upewe kingine ni lazima utoe kiasi cha Tsh. 20,000/= katika Ofisi za NIDA hivyo nawaasa wananchi ukipata kitambulisho hiki tunza vizuri.
Mwisho baraza la madiwani na viongozi wote kwa ujumla wao wanaishukuru sana na kuipongeza Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Mh.Rais Samia.S.H kwa kuwajali wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kuleta fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo katika sekta zote na sasa kazi iendelee.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.