Ilikuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Mbulu wanapata lishe na afya bora, halmashauri ya wilaya ya Mbulu imedhamilia kutokomeza tatizo la utapia Mlo Kwa watoto.
Wataalamu wa Idara ya afya halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakionesha mfano wa darasa mapishi kwa wanakijiji wa Diyomati.
Watumishiwa Idara ya afya wameshiliki kikamilifu katika maadhimishoya siku ya afya kwa kuungana na wananchi wa vijiji vya Diyomat, Hayderer na Dongobesh kutoa elimu ya lishe na darasa la Mapishi bora ili kuandaa lishe na chakula bora kwa mtoto.
Bi. Loveness Mollel- Katibu wa Afya akisisitiza ulaji wa vyakula vya asili kwa wananchi wa Kijiji cha Hyaderer.
“Tatizo la utapia mlo limekuwa ni sehemu kubwa inayoathiri hali ya ukuaji wa mtoto hivyo inatulazimu kama Wataalamu kutoka ofisini na kupita vijijini kutoa elimu ya lishe na darasa la mapishi kwa ufasaha” ameyesema hayo Dr. Ally Fupi Kaimu Mratibu wa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika vijiji vitatu.
Dr. Ally Fupi kaimu Afisa lishe halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akimpatia mtoto moja kirutubisho bora walichokiandaa katika maadhimisho ya lishe kwa wananchi wa dongobesh.
Aidha wananchi wamesisitizwa kuzingatia kanuni na taratibu mbalimbali za lishe zinzotolewa na wataalamu ili kuepukana na tatizo la Utapia Mlo.
Muuguzi - Prisca Mukhay akigawa chakula kwa watoto wa dongobesh waliojitokeza na wazazi wao katika maadhimisho ya lishe
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.