Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mhe. Flatei G. M Akihutubia Katika Sikukuu ya Wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Moses Nduligu Akisalimia Wananchi na Kumkaribisha Mgeni Rasmi
Meza Kuu Wakikagua Mabanda ya Wajasiriamali na Bidhaa Zao
Zoezi la Upandaji Miti kwa Meza Kuu
Bi. Mary Akonaye Mwakilishi Toka Tawi la TALGWU Hospitali ya KKKT Haydom kitoa Mada
Bi. Mchaki Akitoa Mada za Uzazi kwa Akina Mama toka Hospitali ya Wilaya ya Mbulu
Kwa Kadri Muda Ulivozidi Kuyoyoma Ndivyo Mambo Matamu Yalivyozidi Kunoga Uwanjani Hapo, DJ IMA Akiendelea na Utoaji wa Burudani Moja Baada ya Nyingine Katika Sikukuu Hiyo.
~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~
Maadhimisho ya sikukuu ya wanawake duniani yaliyofanyika kiwilaya Kata ya Dinamu Kijiji cha Muslur ambapo Mgeni Rasmi alikua ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mhe. Flatei G. M Tarehe 08.03.2023, kauli mbiu ya mwaka huu ni; "UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA: CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA.
Katika maadhimisho haya elimu ya ukatili kwa akina mama, akina baba na watoto ilitolewa kwa hadhara yote ambapo changamoto ni afya ya akili lakini juhudi za kutatua tatizo hili ni kufika katika Ofisi ya Halmashauri yoyote nchini na kuwaona maafisa ustawi wa jamii ili kuweza kutatua changamoto husika. Akina mama wajawazito wameelimishwa kuwa wanatakiwa kufika kliniki pale tu anapohisi anao ujauzito hii itasaidia kupunguza kasoro mbalimbali zitakazojitokeza kipindi chote cha ujauzito hadi uzazi, kwasababu hali ya maisha na uhimilivu wa magojwa kwa binadamu kwa sasa ni tofauti sana na maisha ya miaka 50 iliyopita.
Hata hivyo katika maadhimisho haya yalisheheni burudani za kukata na shoka mwanzo mwisho zilizolindima uwanjani hapo kiasi cha kupelekea washiriki wote kila mmoja kumwagilia moyo kwa kadri anavyoweza huku milindimo ya pwani, kwaito, bongofleva, zouk na bolingo zikitambaa kwa kishindo katika uwanja wa Kata ya Dinamu uliojaa pomoni. Mashairi, ngoma na kwaya zimeimbwa wakiishukuru serikali katika utoaji wa mikipo ya 10% na kusisitiza serikali na taasisi zisizo za kirerikali kuweza kusaidia maendeleo ya ustawi wa jamii kiwilaya.
Mgeni rasmi alikagua mabanda ya vikundi vya wajasiriamali kama vile kikundi cha SAUMU BASHAY kinachoongozwa na Consolatha Deemay hawa wanasindika vitunguu saumu na kutoa bidhaa mbalimbali, kikundi cha APPLE DIYOMAT kipo Kata ya Dinamu nacho kinasindika bidhaa za zinazotokana na vitunguu saumu. Kikundi kingine ni cha PAMEC ambapo kiongozi wao ni Anne Robert kinachojishugulisha nabidhaa zitokanazo na ufinyanzi na mapambo ambapo wako kata ya Dongobesh, na mwisho ni MELANIA BAJUTA naye yupo kata ya Dongobesh anajishugulisha na uuzaji wa nguo za ndani na mashuka. vikundi hivi kwa ujumla wao wanachangamoto zinazofaana ambazo ni mtaji mdogo na namna ya kupata masoko ya uhakika katika bidhaa zao. Ila Halmashauri imeshawapatia wahusika wote mikopo ya makundi maalumu ya wanawake.
Katika hafla hii kulikuwepo na zoezi la utunzaji wa mazingira kupitia upandaji miti ambapo Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mhe. G.M Flatei alikuwa wa kwanza kisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Joseph G. Mandoo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Mosses Nduligu na Diwani Viti Maalumu tarafa ya Dongobesh Mhe.Kipapai.
MWISHO!
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.