wa Kwanza Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli Akiwa na Maafisa wa TAWESO Bi.Subira Ndutu na Ndg. Mbise B. Anord Ofisini Kwake Katika Kujitambulisha.
wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Ndg. Moses Nduligu, Wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli na Kulia ni Afisa wa TAWESO Bi.Subira Ndutu Katika Kujitambulisha Ofisini Kwake.
Picha za Hapo Juu ni Mafunzo Yakiendelea Katika Ukumbi Mdogo wa Halmashauri
Pakua bango kadhaa hapo chini:-
MBULU DC SEKTA MIFUGO 1 SEC.jpg
~~~~~~~~~~~~~ HABARIKAMILI ~~~~~~~~~~~~~
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu yaliyojumuisha wataalamu wote wa mifugo katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu na wasimamizi wa minada ya Halmashauri kwani nao ni wadau wakuu katika usimamizi wa mifugo minadani na kuona namna mifugo hii inavyoletwa minadani, kuunzwa na hadi kupakiwa kwenye vyombo vya moto kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi, ambapo elimu waliyoipata hapa wataishusha kwa wananchi kupita mihadhara mbalimbali ikiwamo mikutano ya vijiji, minadani na magulioni na sehemu zingine nyingi.
Kwa mafunzo haya itapelekea wananchi mbalimbali kujua taratibu sulihishi za kumfanya mnyama ajiskie huru kama vile kutowekwa juani mda mrefu, kupigwa na fimbo kubwa ikiwa ni pamoja na kuwavuta wanyama mbalimbali kwa nguvu kwa kutumia kamba na pia kipindi cha kuwaswaga kutumia nguvu nyingi hadi wengine kupelekea kuumia. Madhara yake ni kwamba unaharibu ubora wa vitu mbalimbali vinavyodhalishwa kutokana na kuchinjwa mnyama husika au kutoa bidhaa hafifu kama vile maziwa.
Faida ya kutunza wanyama wako; kutoingia kwenye mkono wa sheria ya adhabu ambayo ni sheria ya ustawi wa wanyama ya mwaka 2008, mnyama mwenye afya atauzwa kwa bei ya juu sana awapo sokoni hivyo kukuletea kipato kizuri ukiwa kama mjasiriamali, ambapo kuwasafirisha kwa kutozingatia mazingira bora ya usafirishaji hupelekea baadhi ya wanyama wanaporundikana wengi ambao ni dhaifu hufa njiani na wengine hupata majeraha yanayopelekea mnyama kuteseka na mfanyabishara kupata hasara ya kupungua kwa idadi ya mifugo aliyonayo, kwa hiyo wataalamu hawa wanasisitiza kuwepo kwa miundombinu rafiki kwa ajili ya wanyama wote
Kimsingi TAWESO ni shirika lisilo la kiserikali ambalo makao maku yao yapo Dar es salaam wakifanya kazi hizi kwa msaada wa shirika la Welttierschutzgesellschaft (WTG) la nchi ya Ujerumani, kwa mawasiliano ni 0713 322796 / 0752 660101 au kwa barua pepe info@taweso.org na katika tovuti ni www.taweso.org
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mbulu Ndg. Abubakar A. Kuuli ameishukuru Taasisi hiyo ya TAWESO kwa elimu hii kwa wataalamu wake kwani itakuwa chachu ya kutumia njia bora ya kutunza na kusafirisha wanyama hawa ambapo kwa halmashauri ya mbulu mifugo na minada ni mingi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.