Wataalamu wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya Wakiwa Kwenye Kikao Kazi cha Mafunzo ya UVIKO 19 Kilichofanyika Katika Ukumbi wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania Mbulu Mjini.
Kutoka Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Dr. Pellagia Shirima na Anayefuata ni Katibu wa Idara ya Afya Wilaya Bi. Monica Shauri
Wataalamu Hao Wakiwa Katika Mafunzo Kwenye Ukumbi Huo
Katika Kikao Hicho Aliyesimama ni Mratibu wa Njanjo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Ali Suleman Ali
MBULU MAFUNZO CHANJO 30.07.2022.jpg
~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~
Katika kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na taifa kwa ujumla kuwa salama na maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19 ili kuwafanya wananchi waendelee kufanya kazi zao za kiuchumi na kijamii bila shida, kumefanyika mafunzo maalumu ili kuongeza kasi ya uchanjaji miongoni mwa jamii. Malengo mahususi ya mafunzo haya ni Kufahamu majukumu mbalimbali wakati wa kutoa chanjo, Kujadili jinsi ya kutoa chanjo wakati wa kampeni na Kufahamu ujumbe muhimu kwa jamii wakati wa utoaji wa chanjo.
Timu hiyo inajumuisha wataalamu wa afya makao maku ya Halmashauri ya Mbulu, Maafisa tehama katika kutoa msaada wa kiufundi katika mfumo wa usajiri wa UVIKO 19, hata hivyo wataalamu wa vituo vyote vya kutolea huduma ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu katika kata zote zipatavyo 18 ambapo huu ni mkakati wa kimkoa katika Halmashauri zote kuhakikisha wananchi wanachanjwa kwa 40% hadi tarehe 08.08.2022 na 70% desemba 2022 lakini hadi tarehe 28.07.2022 kimkoa ilikuwa ni 32%.
Katika mafunzo hayo walikuwepo wawakilishi toka Wizara ya Afya, Mkoa wa Manyara na watalaamu kutoka Shirika wahisani la Japani JHPIEGO kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Imefahamika hadi sasa ugonjwa wa UVIKO 19 bado upo hivyo kila mwananchi ajikinge kwa kila njia kama vile kunawa mikono kwa maji tiririka na vitakasa mikono "sanitizer" , kuvaa barakoa, kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu, kuziba mdomo wakati wa kukohoa kwa kiwiko cha mkono na endapo ukihisi dalili zozote za UVIKO 19 basi fika kituo cha kutolea huduma kilichokaribu kwa ajili ya kupata matibabu au toa taarifa kwa ndugu na majirani wakusaidie. Dalili za uviko-19 ni pamoja na: homa, kikohozi, mafua, kuchoka mwili, kukosa pumzi, maumivu ya misuli ya mwili mtu yeyote anaweza kupata maambukizi ya ugonjwa huu. watu walio na umri zaidi ya miaka 60 na wale wenye magonjwa mengine mfano kisukari, shinikizo la damu na mengine mengi wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu na kupelekea kifo.
katika kampeni hii ya lipa kwa matokeo vituo vyote vya kutolea huduma ya afya vitakuwa vitatoa huduma hii ya kuchanja na wengine watakuwa wakitembea nyumba kwa nyumba. Aina ya chanjo zilizopo ni Janssen n Jansseni ambayo ni ya dozi 1 na Sinopharm ya dozi 2 tu zote hizi ni salama kwa afya yako.
Mteja anaweza kujisajiri ili kubuku "booking" yeye mwenyewe na wapi anahitaji achanjwe kupitia mtandaoni kiganjani mwake katika kiunganisi hiki https://chanjocovid.moh.go.tz ambapo imefahamika kwamba inafanya vizuri zaidi kupitia vivinjari "browsing software"aina ya mozzira, google chrome na opera, lakini hata kama muhusika hawezi kufanya yote haya mlango uko wazi fika moja kwa moja katika kituo cha kutolea huduma ya afya utasajiriwa hapo na kupata huduma hapo hapo. Uwepo wa mifumo hii unamuwezesha mwananchi kuomba na kupata huduma popote Tanzania na wataalamu wa afya huangalia ripoti mbalimbali na kufanya maamuzi kulingana na namana yalivyoombwa kwenye mfumo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.