Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akizungumza Katika Mahafali Hayo.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akiingia Shule ya Sekondari Philip Marmo Akipokelewa na Wenyeji Wake Mkuu wa Shule Bw. Edmund E. Obed na Afisa Mtendaji wa Kata ya Endamilay (wa kike kushoto) Bi. Natalia Julius.
Wanafunzi wa Kidato cha 4 Wakiingia kwa Muziki Maalumu Eneo la Sherehe Katika Mahafali Hayo Shule ya Sekondari Philip Marmo.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akisoma Vitu Mbalimbali Katika Mahafali Hayo.Wanafunzi wa Kidato cha 4 Katika Mahafali Hayo.Wananchi Wakiwa Katika Mahafali Hayo.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikagua Kikosi cha Skauti cha Shule Hiyo.
Bw. Mussa Mpinga Mzee Aliyewawakilisha Wazazi kwa Upande wa Wanaume Kuzungumza Neno la Heri kwa Niaba Katika Mahafari Hayo.
Bi. Pepetua Philipo Aliyewawakilisha Wazazi kwa Upande wa Wanawake Kuzungumza Neno la Heri kwa Niaba Katika Mahafari Hayo.
Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Ukakamavu wa Skauti katika Kusimamisha Pikipiki Kutokutembea.
Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kucheza Muziki wa Miondoko ya Kizazi Kipya.
Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kitaaluma Namana ya Kutambua Chakula Kama Kina Protini Kwa Kutumia Vifaa Maalumu Vya Somo la Kemia Wako Vizuri kwa Kweli na Hii ni Pongezi Kubwa Sana kwa Waalimu.
Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Kucheza Muziki wa Mirindimo ya Kitamaduni Zaidi.
Wanafunzi Wakiwa Katika Maonyesho ya Skauti wa Mbele ni Kiongozi Wao Foibe D. Joseph.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Zawadi ya Tsh. 120,000/= kwa Wanafunzi Hao Walionyesha Michezo Mbalimbali.
Wanafunzi Wakibeba Keki .
Wanafunzi Wakikabidhi Keki kwa Mkuu wa Shule Bw. Edmund E. Obed
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Alivishwa Vazi la Heshima la Kimila na Fimbo ya Kimila ya Kiiraq.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Cheti cha Pongezi kwa Mkuu wa Shule ya Philip Marmo Bw. Edmund E. Obed.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akikabidhi Cheti cha Pongezi kwa Mwalimu wa Michezo Bi. Doroth Baraka wa Philip Marmo.
Wanafunzi Wakikabidhiwa Vyeti.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Katika Picha ya Pamoja Waalimu na Wanafunzi.
Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Abubakar A. Kuuli Akiondoka Baada ya Kuisha Mahafali Hayo.
~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri jana katika mahafali yaliyofana kwelikweli kwa kuambatana na maonyesho mbalimbali ya vichekesho na kuelimisha umma kama vile igizo lililo elimisha wazazi kutoendelea kushikilia mila na desturi potofu za kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo na kuacha masomo, pia ukeketaji ambao humuathili mwanamke katika uzazi namna ya kujifungua kwa kupata maumivu makali na kutokwa na damu nyingi na hata kupelekea kifo.
Onyesho la kitaaluma lililowahusisha wanafunzi 5 ambao waliandaa jaribio la namna ya kutambua kama chakula husika kina protini jambo ambalo lilithibitika baada ya mchanganyiko wa kemikali kadhaa na chakula husika kuonyesha rangi ya bluu iliyokolea. Huu ni uwezo tosha kwa wanafunzi hawa kuwa wataalamu wa kuchambua vyakula mbalimbali vinavyotumika na binadamu ili kujua kama vina madhala au la!
Maonyesho ya ukakamavu ya kikosi cha skauti yaliyofundisha kwamba kila jambo likifanyiwa kazi vya kutosha kwa kujituma basi linawezekana kufanikiwa, imefahamika wazi kwamba vipaji vya watoto kutoka kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Sekondari ya Philip Marmo ni vya kiwango cha juu kabisa.Shule ya Sekondari Phili Marmo iko kata ya Endamilay na ilikuwa na wanafunzi 82 kutokana na sababu mbalimbali imepelekea hadi sasa kuwa na wanafunzi 75 ambao ndiyo watakaofanya mtihani wao wa kitaifa wa kidato cha 4 katikati ya mwezi Novemba 2021.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar A.Kuuli amesifu vipaji mbalimbali walivyonavyo wanafunzi hawa na kutamka viendelezwe, hakuishia hapo tu aliwatunuku kiasi cha Tsh. 120,000/= kwa wanafunzi 12 wa uimbaji. Lakini amewashukuru waalimu wote walioshiriki katika uleaji wa vipaji hivi kwani ni hazina kubwa kwao na jamii kwa ujumla. Kwa sasa uwekezaji katika michezo, burudani na sanaa za maonyesho ni sehemu tosha ya kujipatia kipato cha juu kama ilivyo kwa watu mbalimbali waliofanikiwa kupitia kada hizi hivyo wasikate tamaa.
Mgeni rasmi huyo aliendelea kusisitiza kwamba "ni lazima wanafunzi kuwa na tabia njema ndiyo mwanzo mzuri wa mafanikio yoyote, hivyo muepuke kuwa wezi, wabakaji, tabia mbaya na kuwasaidia wazazi katika kazi mbalimbali pale inapofaa kufanya hivyo, lakini pia mshikeni sana MUNGU kwani yeye ndiyo kila kitu" alisisitiza.
Kuhusiana na changamoto za maabara, bweni na bwalo Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw.Abubakar A.Kuuli amesema atamtuma Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Mbulu kuja kufanya tathmini ya kiasi gani kinahitajika katika kila mradi na litaandikwa andiko kwenda kwa wadau mbalimbali kama vile (TEA) wanaotusaidia katika fedha mbalimbali za Elimu, pia kwa ujio wa Mhandisi atasaidia kazi zilizokuwa zimesimama kwa muda mrefu ziweze kuendelea, kwani fedha zipo. Mhandisi atakuja wiki ijayo kuanzia tarehe 18.10.2021 lakini kuhusu maji atawasiliana na Meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini (RUWASA) ili nao wafike wafanye tathmini kisha tutajua tutakabiliana vipi na hiyo gharama itakayoletwa ili maji yafike hapa Shuleni Philip Marmo sekondari.
Hata hivyo ukosefu wa vifaa TEHAMA kama vile kompyuta (Tarakilishi) na printa (kinakilishi) kwa ajili ya kufanyia kazi mbalimbali za kimfumo kuanzia FFARS mfumo wa malipo, PREM usajili wa wanafunzi na SELFOM mfumo wa uhakiki wanafunzi hususani katika ngazi ya kufanyia mitihani. Katika kujibu hili hapa Mgeni rasmi alitamka kwamba fedha elimu bure zinazoingia kila mwezi basi waangalie namna ya kutumia fedha zile katika ununuzi wa Vitanda na vifaa tehama hivi lakini na yeye atasaidia ununuzi wa PRINTA.
Mgeni rasmi huyo alitamka kwamba "mtoto yeyote wa kike ambaye atashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa fedha za kuendelea na elimu yake basi afike kwa Mkuu wa shule hii kisha mimi Mkurugenzi mwenyewe nitaangalia namna ya kumsomesha mwanafunzi huyo".
Mgeni rasmi amewashukuru wanafunzi, wazazi, viongozi wa dini, chama, waalimu na wanafunzi kwa ujumla wao kwa ushiriki wao katika mahafali haya.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.